319 views 2 mins 0 comments

BODI YA FILAMU KUANDAA TENA TUZO ZA FILAMU

In BURUDANI, KITAIFA
August 11, 2023

Bodi ya filamu imefungua dirisha la kupokea filamu Kwa ajili ya tamasha la Tuzo za filamu 2023 Tanzania ikiwa Moja wapo ya tamasha hilo ambalo linalokuza filamu za kitanzania na kuzidi kuleta chachu ya kuendeleza vipaji vya Sanaa

Tuzo hizo zimekuwa msimamo wa mbele ambazo ndizo zinazoweza kukutambulisha kazi yako unayoifanya ya kutunga au kucheza filamu hizo Ili kuzidi kushindana na kutengeneza filamu zenye ubola ndani ya nchi au nje ya nchi

Akizungumza na waandishi wa habari Katika ufunguzi huo jijini Dar es salaam Katika ukumbi wa new Africa Leo ijumaa 11 august 2023 katibu mtendaji wa bodi ya filamu Tanzania Dkt.Kiagho kilonzo amesema lengo la uwepo wa Tamasha la Tuzo hizo ni kutambua mchango wa wasanii na wadau wote wa filamu Katika eneo hili la filamu, kutambua vipaji vyao,kuwaongezea hamasa ya kuzalisha kazi zenye ubora zaidi Ili wawe na ushindani mkubwa ndani na nje ya nchi, na kusisimua fursa za uwekezaji Katika eneo hilo la filamu Nchini.

Zoezi la upokeaji filamu zitakazoshiriki Katika Tamasha la Tuzo za filamu Tanzania 2023 Limeanza rasmi tarehe 11 agosti 2023 ambapo filamu zitapokelewa Kwa njia tatu ikiwemo,kuwasilishwa ofisi za bodi Kwa njia ya mtandao, https//taffa. info (mfumo utafunguka tarehe 17Aug) pamoja na kuzifuata filamu mikoani Katika mikoa 26 Tanzania bala

Pamoja na mambo mengine tamasha la Tuzo za filamu Tanzania 2023 limeongeza wigo wa ushiriki wa filamu kutoka nchi za Afrika mashariki ambazo zimeandaliwa Kwa lugha ya kiswahili Ili kuendelea kuithamini na kuikuza lugha hiyo ambayo ni Moja ya nembo ya Taifa letu

Baadhi ya wasanii wakitoa maoni Yao kuhusu Tamasha hilo linalotarajia kuanza siku SI nyingi Kwa kuanza mchakato wa kuzipeleka Bodi ya filamu
Katibu mtendaji wa bodi ya filamu Dkt.kiagho akizungumza na wasanii hao ambao wamejumuika Kwa pamoja Kwa kujiandaa na Tamasha la Tuzo za bodi ya filamu

Madina Mohammed

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram