Muuguzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mawengi Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, Ubatizo Sanga mwenye umri wa miaka 55 amefariki baada ya kupigwa na mchi wa kinu kichwani na baadaye kubakwa na Mtoto wake Asifiwe Haule mwenye umri wa miaka 25.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amethibitisha kutokea kwa tukio hilo August 08,2023 majira ya saa 10 jioni ambapo amesema tayari Mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na kwamba taarifa zaidi juu ya tukio zitatolewa na Polisi.
DC Victoria amesema “Nimetoka kuongea na Kaimu OCD ameniambia hilo tukio kwa kina na huyo Mhusika tayari yupo chini ya ulinzi, usalama unaendelea kuimarishwa kwani tukio limetokea ndani ya Familia husika, kubwa kama huyu Mtu angekuwa hajakamatwa ina maana ingeweza kuleta shida kwenye Jamii lakini ni Mhalifu ambaye ameshakamatwa”
Awali Mwenyekiti wa Kijiji cha Mawengi Renatho Kahako alisema kuwa Mtoto huyo alifanya mauaji ya Mama yake na baadaye akaibaka maiti “Huyu kijana ni kama alikuwa amechanganyikiwa muda mrefu, kidogo alikuwa hayupo timamu.