291 views 32 secs 0 comments

SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA TAEC

In KITAIFA
August 09, 2023

Waziri wa kilimo Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mh.SHAMATE SHAAME KHAMIS amesema serikali inathamini kazi inayofanywa na Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) katika kudhibiti matumizi salama ya mionzi nchini.

SHAMATA ameyasema hayo baada ya kutembelea banda la Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) katika maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayoendelea Jijini Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale.

SHAMATA amesisitiza kwamba makontena mengi yanaingia nchini kupitia bandari zetu hivyo udhibiti wa mionzi unahitajika ili kuhakikisha wananchi na mazingira yanakuwa salama.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania PETER NGAMILO amesema wanashiriki maonesho ya nane nane ili kutoa elimu kwa wananchi namna taasisi hiyo inafanya kazi hususani kusaidia watafiti katika sekta ya kilimo ili kupata mbegu bora za kilimo.

“Kwa kutumia teknolojia ya nyuklia tumefanikiwa kuwawezesha watafiti wa kilimo na wakatengeneza mbegu ya mpunga inayoitwa Super BC ambayo inatumika Zanzibar hivi sasa na matokeo yake ni mazuri, inatoa hadi tani saba kwa hekari moja” amesema Peter.

Maonesho ya nanenane kitaifa yanatarajiwa kuhitimishwa Agosti 08 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mh. Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1212

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram