255 views 3 mins 0 comments

NAIBU KATIBU MKUU DKT.HUSSEN ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU NANE NANE MBEYA

In KITAIFA
August 06, 2023
Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo Dkt.Hussen Omary akioneshwa nakala ya Sheria ya Usimamizi wa maafa Na.6 ya mwaka 2022 na Mratibu wa maafa Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri mkuu Bi.Numpe Mwambenja alipotembelea Banda la ofisi hiyo Katika maonesho ya kilimo kimataifa maarufu Nane Nane yanayoendelea Katika viwanja vya john Mwakangale jijini MBEYA
Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo Dkt.Hussen Omary akiuliza jambo Kwa afisa mkuu mawasiliano na uhusiano kwa umma kutoka kwenye programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili (ASDP II) ofisi ya waziri mkuu sera, Bunge na Uratibu Bi.Rachel Lugoe wakati alipotembelea Banda la ofisi hiyo Katika maonesho ya nane nane mbeya
Mratibu wa Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya waziri mkuu Dkt.Henry Kissinga akitoa maelekezo Kwa wanafinzi kuhusu Masuala ya afya pale walipotembelea Katika Banda la ofisi hiyo Katika maonesho ya nane nane yanayoendelea jijini MBEYA
Mratibu kutoka Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Bi.Mwansiti Omary akitoa maelezo Kwa Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo Dkt.Hussen Omary alipotembelea Banda la ofisi ya waziri mkuu sera,Bunge na Uratibu wakati wa maonesho hayo
Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo Dkt.Hussen Omary (kulia) akioneshwa picha ya muonekano sahihi wa Bendera ya Taifa,anayemuonesha ni mpigachapa msaidizi mwandamizi Bw.Mrebo Jorwa (Kushoto) alipotembelea Banda la ofisi ya waziri mkuu wakati wa maonesho ya nane nane jijini MBEYA
Mratibu WA Ukimwi MKOA wa mbeya Bw.Emmanuel Petro akitoa elimu ya Masuala ya ukimwi Kwa Vijana walioko kwenye mradi wa Dream waliotembelea Banda la ofisi ya waziri mkuu sera,bunge na uratibu wakati wa maonyesho ya kilimo ya kimataifa nane nane jijini MBEYA
Afisa mkuu mawasiliano na uhusiano kwa umma kutoka Katika programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) ofisi ya waziri mkuu sera, bunge na uratibu Bi.Rachel Lugoe akitoa elimu Kwa wanafunzi waliotembelea Banda la ofisi hiyo wakati wa maonesho ya nane nane jijini MBEYA
Mratibu wa maafa Idara ya menejimenti ya maafa ofisi ya waziri mkuu Bw.Khowe Malegeri akieleza kuhusu shughuli za uratibu wa maafa Kwa Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo Dkt Hussein Omary alipotembelea Banda hilo wakati wa maonesho ya nane nane

Kauli mbinu ya maonesho hayo ni “Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo Endelevu ya chakula

Madina Mohammed

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram