252 views 45 secs 0 comments

TBA WATEKELEZA MRADI WA MAGHARA YA KUHIFADHIA CHAKULA MIKOA NANE TANZANIA

In KITAIFA
August 05, 2023

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) umetekeleza Miradi wa Maghara ya kuhifadhia chakula katika Mikoa Nane ya Tanzania ili kuwasaida wakulima kuhifadhia mazao yao.

Miradi hiyo ni ya teknolojia ya kisasa na inatekelezwa katika Mikoa hiyo ili kusaidia utunzaji wa mazao ya wakulima na kuongeza kuwa mikoa hiyo ni pamoja na ya Nyanda za Juu kusini, ambayo ni Songea, Songwe Makambako, Sumbawanga, Katavi, Shinyanga Manyara na Mkoa wa Dodoma.

Mhandisi wa mradi Haruna Kalunga amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Agost 4,2023 walipotembelea banda la Wakala wa majengo Tanzania TBA Kwenye sherehe za maonesho ya kimataifa ya kilimo Nane Nane 2023.

Mhandisi Kalunga amebainisha kuwa mradi wa ghala la kuhifadhia chakula Sumbawanga umeanza kutekelezwa mwezi Januari 2020 na umekamilika mwezi Machi 2023 na umeanza kutumika kwa kuhifadhi mazao ya chakula kwa Wakulima.

“Mradi wa Sumbawanga ni wa teknolojia ya kisasa, na unatunza chakula cha walicholima wakulima Tani 21,000 na lengo kuu la mradi huo kutekelezwa kwa Mikoa 20 lakini kwa sasa tumeanza na Mikoa Nane,” amesema Wakala wa majengo Tanzania mhandisi Haruna Kalunga.

Aidha Mhandisi Kalunga alitumia nafasi ya wanahabari hao kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo na kufika katika banda la TBA ili kujua mambo mbalimbali ikiwemo gharama za ujenzi pamoja wa nyumba za makazi na taasisi za serikali kwa ghalma nafuu.

/ Published posts: 1588

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram