
Tanzania yatajwa ni nchi ya pili Afrika Kwa kuwa na ongezeko kubwa la watalii Katika robo ya kwanza ya mwaka 2023 na Nchi ya kwanza inayofatia ni Ethiopia na ya tatu ni Morocco
Pia Tanzania ni nchi ya pili kuingia ushiriki wa mkutano wa shirika la UN la utalii Kanda ya Afrika (UNWTO-CAF) Katika ushirikiano huo unaendeleza kukuza na kuendeleza sekta ya utalii nchini
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katika ofisi za bodi ya utalii Leo jumamosi 05 august 2023 katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii Dkt.Hassan Abbas amesema utalii unabaki kuwa miongoni mwa sekta muhimu za kiuchumi hapa Nchini sekta hiyo ndio chanzo kikubwa Cha fedha za kigeni ambapo inachangia asilimia 25 ya fedha zote za kigeni nchini
“Katika kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kuupeleka utalii wetu kimataifa kupitia filamu ya “Tanzania The Royal Tour”Moja ya mikakati ya wizara Kwa Sasa ni kuimarisha ushiriki wetu Katika vyombo mbalimbali vya kimataifa Ili kuendelea kubadilishana uzoefu kujitangaza kimataifa pamoja na kukuza ushirikiano wa kimataifa”.Amesema Abbas
UNWTO ni shirika la umoja wamataifa ya utalii duniani lililoanzishwa tangu mwaka 1974 mpaka Sasa shirika hilo Lina wanaChama washirika ambao hukutanisha wadau wa utalii Zaidi ya 500 Dunia shirika hili Lina Kanda 6 za mabara ya Dunia ikiwemo Afrika.
“Tanzania ni mwanachama kamili wa shirika hilo na pia ikitekeleza majukumu yake na shughuli mbalimbali za shirika hilo ikiwemo kulipa ada ya uanachama ya kila mwaka kushiriki vikao na maazimio yanayotolewa na UNWTO”Akibainisha Abbas
Aidha amesema Katika kuiwakilisha nchi waziri wa maliasili na utalii mhe.mohammed mchengerwa ataliwakilisha bara la Afrika Katika nafasi ya Makamu wa RAIS kwenye Mkutano mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la utalii duniani UNWTO Kwa kupitia nafasi hiyo ya kutangaza vivutio vyetu.
Madina Mohammed