224 views 2 mins 0 comments

HARAMBEE YA KUCHANGIA WATOTO WALEMAVU YAJA KWA KISHINDO

In KITAIFA
August 04, 2023

Taasisi ya Dayosisis ambayo inayolea watoto walemavu na wasiojiweza ambayo anakabiliwa na changamoto ya miundombinu mbalimbali ikiwemo uchakavu na ukosefu wa vitendea kazi.

Taasisi hiyo inafanya harambee Kwa ajili ya kuwasaidia watoto walemavu ambao wasioona na wale wenye utindio wa ubongo na akili, harambee hiyo itafanyika mlimani city na mgeni rasmi atakuwa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania RAIS Samia Suluhu Hassan

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo ijumaa 04 august 2023 Askofu Msafiri Adof Amesema taasisi yet inavituo vingi na inaukosefu wa vitendea kazi vipo hafifu na inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo pia ukosefu wa vitendea kazi Kwa shule ya vilente ya watoto wasioona na miundombinu imechakaa vya kufanyia kazi Kama breed mashine na mashine hiyo inagharimu milioni 80

“Vituo hivi vinakabiliwa na madeni makubwa ndo maana tumeona tufanye harambee kubwa Kwa ajili ya kupata fedha zitakazosaidia kuimarisha vituo hivyo viweze kufanya kazi ya mungu”. Amesema Adof

Aidha Katika taasisi yetu Kuna vituo ambavyo vinaumri vya miaka 100 taasisi hiyo ameazishwa mwaka 1890 tokea walivyoingia wamisionali ambao walianzisha vituo vikubwa.Hospital ya wagonjwa wa akili ya kwanza Afrika mashariki iliyopo utindi na kituo Cha watoto wasioona kipo ilente

Hata hivyo amesema Kuna kituo Cha watoto yatima kilichopo ilente Dar es salaam kituo hicho kinauwitaji wa misaada mbalimbali na kituo hicho kinapokea watoto wa aina zote na dini zote

Nae Mratibu wa harambee Steve Nyerere amewaomba mataasisi makampuni wanasiasa kuweza kuunga mkono jambo hilo la kuchangia harambee Kwa watoto na uhitaji wasioona Ili kuweza kukuza mahitaji Yao muhimu wanayohitaji

“kwani jambo hili SI la mtu mmoja ni la watanzania wote tushikane mkono kuwasaidia watoto wetu kwani wanateseka sana Kwa kukosa vitendea kazi tushikane na kuwasaidia kwani Rais wetu mama samia nae anapambana kuwasaidia watanzania wote”Amesema Nyerere

Madina Mohammed

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram