
KAMA sehemu ya juhudi za Ghana za kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya Ghana na Tanzania chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA), Ofisi ya Kitaifa ya Uratibu wa AfCFTA ya Ghana (NCO) imepanga kufanya msafara wa kibiashara kwenda nchini Tanzania Septemba 25 na 26, 2023.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa juma lililopita wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Ofisi ya Kitaifa ya Uratibu wa AfCFTA ya Ghana Dkt. Fareed Arthur alisema kwamba Ghana imekuwa na uhusiano mkubwa na Tanzania, tangu wakati ambapo marais waasisi Dkt. Kwame Nkuruma na Mwalimu Julius Nyerere walishirikiana katika harakati za kupigania uhuru wa Afrika.
โWakati viongozi hao wawili wakiongoza harakati za kupigania uhuru wa kisiasa ni imani yetu kuwa AfCTFA inashikilia ufunguo wa ukombozi wa kiuchumi na ukombozi wa Afrika. Ni ujumbe huu, ambao umeirudisha NCO katika Jiji hili la kihistoria la Dar es Salaam,โ alisema Dkt. Arthur.
Dkt. Arthur alieleza kuwa msafara huo wa kibiashara utakuwa wa pili mfululizo, kufuatia msafara wa hivi karibuni uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.
“sisi sasa tuko tayali na hata hivyo tumeshaanza Utekelezaji na hitifaki za kibiashara la soko kuu la Afrika Hadi Sasa tumeshatoa vibali Zaidi ya vitano unavyoenda Katika mataifa ya kaskazini ya Afrika lakini pia na Afrika magharibi ikiwa Ghana ni Moja ya nchi ambazo tunafikiri Kwa hii fursa Kwa kuja kuwa na maonesho hapa inaweza ikatupa nafasi wafanyabiashara wa nchi yetu kuwa na fursa za kimasoko na kimashirikiano ya kibiashara”. Amesema Arthur

Alibainisha kuwa kwa kuzingatia kukuza ushirikiano wa kibiashara, kuchunguza matarajio ya biashara, na kukuza fursa za Uwekezaji Kati ya Nchi hizi mbili, tukio hilo linaahidi kuwa uzoefu wa kurutubisha makampuni ya Ghana na Tanzania.
Ameeleza kwamba kwa maonesho hayo ya Ghana 2023, Tanzania itatoa jukwaa madhubuti kwa viongozi wa Sekta, wavumbuzi, wajasiriamali na watunga sera kutoka Ghana na Tanzania na sehemu nyinginezo za Afrika Mashariki kufanya Kazi pamoja kutafuta fursa za mabadiliko ya Viwanda na kukuza biashara kwa manufaa ya wananchi wa Nchi hizi mbili.
Kwamba programu hiyo ya kina kwa muda wa siku tano za maonesho hayo itahusisha maonesho ya bidhaa za Ghana na Tanzania, Semina na mijadala ya Watu mashuhuri kutoka Ghana na Tanzania kuhusu maendeleo ya kiuchumi na kuimarisha uhusiano Kati ya Nchi hizi mbili.
Pia ametoa wito Kwa wafanyabiashara kw tarehe hiyo 25 na 26 September mlimani city waje kuona fursa ambazo watakazo ziweza kufanya naa taifa la Ghana na wanakaribishwa wafanyabiashara wa Ghana tutashirikiana nao Kwa pamoja na kuhakikisha tukio hili linafanikiwa likilenga hasa wafanyabiashara katika mataifa haya mawili na Afrika Kwa ujumla
Madina Mohammed