307 views 2 mins 0 comments

MKESHA WA MWENGE WA UHURU 2023 KUAMBATANA NA KUSHEREKEA MAFANIKIO YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

In KITAIFA
July 29, 2023

Mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2023 kuambatana na kusherekea mafanikio ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Fack Lulandala amesema usiku wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2023 katika Halmashauri ya Mji Tunduma itakuwa ni sherehe kubwa ya kusherehekea mafanikio ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania kwa kipindi cha uongozi wake.

Mkuu wa Wilaya ya Momba, Mhe. Fack Lulandala amesema usiku wa mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2023 katika Halmashauri ya Mji Tunduma itakuwa ni sherehe kubwa ya kusherehekea mafanikio ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania kwa kipindi cha uongozi wake.

Mkuu wa Wilaya, Mhe. Fack Lulandala amesema hayo wakati wa kikao kazi cha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2023 kilichofanyika ukumbi wa High Class na kuwakutanisha wadau wa maendeleo wa Mji wa Tunduma wakiwemo Madiwani, wafanyabiashara, vikundi mbalimbali, walimu Wakuu na Wakuu wa Shule pamoja na viongozi wa Mila, mitaa na Kata.

Mwenge wa Uhuru utapokelewa Septemba 5 kutoka Wilaya ya Mbozi na mkesha wa sherehe za mafanikio ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan zitafanyika Mpemba septemba 5.

Mhe. Fack Lulandala amesema Katika kufanikisha sherehe hii ya mafanikio ameunda kamati za maandalizi ambazo zinaundwa na wananchi wa Tunduma pamoja na watumishi.

“Nimeamua kuunda Kamati ambazo wananchi ndio wengi kuliko watumishi kwa kuwa Mwenge wa Uhuru ni mali ya wananchi na sio watumishi tu na sherehe ambayo tunaiandaa ya mafanikio ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inahusu mafanikio makubwa ambayo wananchi wa Tunduma wamepata kwa kipindi chake” Mhe. Fack Lulandala.

“Nimeielekeza Kamati ya maandalizi ya Mwenge wa Uhuru kuhakikisha siku hiyo burudani nzuri inakuwepo kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa tunataka siku ya mkesha wa Mwenge wa Uhuru iwe ni Sherehe ya kuambatana na burudani nzuri kwa wananchi wote wa Tunduma” Mhe. Fack Lulandala.

Pia, Mkuu wa Wilaya, Mhe. Fack Lulandala ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru pale Mpemba, sehemu utakapokesha pamoja na kwenye miradi utakapokuwa unapita.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Tunduma, Mhe. Ayubu Mlimba amesema wao madiwani watakwenda kuwahamasisha wananchi washiriki kwa wingi kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru.

Editor / Published posts: 21

Journalist

Twitter
Facebook
Youtube
Linkedin
Instagram