136 views 2 mins 0 comments

TIGO KUINGIA UBIA TENA NA AZANIA BANK

In BIASHARA
July 27, 2023

Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tanzania, Tigo, imezindua mfumo wa bidhaa yake ya mikopo iliyoboreshwa kupitia Tigo Pesa kwa kushirikiana na Benki ya Azania.

Uzinduzi huu imezinduliwa Leo Alhamis 27 2023 Katika ukumbi wa Serena hotel Jijini Dar es salaam ambapo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha upatikanaji wa mikopo ya muda mfupi iliyopo na kukuza ushirikishwaji wa kifedha nchini Tanzania ambayo kwa sasa imesajiliwa kwa asilimia 76%.

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Mtendaji Mkuu wa Tigo Pesa, Bi Angelica Pesha amesema Tunafuraha kuleta sokoni bidhaa ya mikopo iliyoboreshwa ya Nivushe Plus kwa kushirikiana na benki ya Azania kama sehemu ya mkakati wetu wa kuwawezesha wateja wengi zaidi kutumia huduma rasmi za kifedha kupitia simu zao za mkononi ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku kwa urahisi.


“Huduma ya Nivushe Plus kama bidhaa iliyoboreshwa ya mkopo kupitia simu za mkononi ni huduma ya kwanza ya mkopo nchini Tanzania ambapo Tigo inatarajiwa kushirikiana na benki mbalimbali kutoa mikopo maalum kwa wateja wa Tigo Pesa wenye sifa”. amesema pesha

Huduma ya mkopo ya Nivushe Plus itawasaidia wateja wa Tigo Pesa kupata manufaa ya ziada ambayo ni pamoja na kupata kiasi kikubwa cha mkopo ikilinganishwa na vipimo vya awali vya mkopo. Kwa hiyo, wateja sasa wanaweza kukopa hadi TZS 2,000,000/-. hapo hapo kutegemeana na pointi zao za ukopaji ambazo zinakokotolewa kutokana na matumizi yao ya huduma za Tigo Pesa.


Nae Mkuu wa Kitengo cha Benki Kidijitali (Digital Banking) wa benki ya Azania, Vinesh Davda, ametoa maoni yake kuhusu ushirikiano na kampuni ya Tigo.

โ€œTunafuraha kushirikiana tena na Tigo Pesa katika jitihada za kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma za kifedha nchini Tanzania. Kwa kuunganisha utaalamu wetu wa kibenki na mtandao mkubwa wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi Tigo Pesa na ari ya uvumbuzi, tunatengeneza ushirikiano wenye nguvu ambao utaleta mapinduzi katika utoaji wa mikopo midogo midogo.โ€ amesema Davda


Mafanikio ya Tigo Pesa kufikia kuwa mtoa huduma kamili wa huduma za kifedha yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ubunifu na mtandao madhubuti kufuatia mpango unaoendelea wa kuboresha mtandao ambao umewezesha upatikanaji wa huduma za Tigo Pesa nchini kote.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram