305 views 21 secs 0 comments

MWANAHARAKATI OSAKA APINGA VIKALI TUKIO LA KUSHAMBULIWA KWA WANAHABARI WA WANANCHI

In KITAIFA, Uncategorized
July 26, 2023

Wanaharakati wa kujitegemea wa kutetea haki za binadamu Deusedith Isaac Soka
Amelaani vikali Kwa wale ambao walioweza kufanya vurugu Katika mkutano wa chadema ambao uliofanyika Katika viwanja vya temeke buriaga Kwa kushambuliwa Kwa waandishi wa habari wa mwananchi

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo jumatano 26 julai amesema gari ya wananchi ilifaanyiwa uharibifu kwa kushambuliwa Kwa kuvunjwa vioo na kuchukuliwa simu zao

“ninalaani Kwa nguvu zote kushambuliwa Kwa vyombo vya habari vikiwa vinatekeleza wajibu wao kule ni kushambuliwa Demokrasia”.

“Hivyo basi kutokana na kitendo walichokifanya Vijana wenzetu ni swala la kinyama kwani Kwa kutumia silaha zenye ncha Kali na marungu waliweza kuwaumiza waandishi wa habari pamoja na sisi Vijana tuliokuwa tunaratibu mkutano uliofanyika 23 julai 2023 Viwanja vya temeke buriaga”. Amesema Osaka


Aidha Osaka amesema Msimamo wetu kama wanaharakati katika Suala hili ni kujali uhuru na kulinda sheria zetu pamoja na kulinda amani ya nchi yetu Tanzania, Tutawapeleka Mahakamani vijana wote waliohusika kutekeleza shambulio kwetu sisi na waandishi wa habari.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram