456 views 40 secs 0 comments

WANAWAKE BUTA VICOBA WATAKIWA KUTOKUWA NA UBINAFSI

In KITAIFA
July 25, 2023

Kikundi Cha Buta Vicoba Endelevu kimezinduliwa rasmi Jana na Mwenezi wa CCM Kata ya Bunju Shabiri Akbal Ismail na kuwataka wanawake hao kuwa pamoja na kushirikiana Kwa kila jambo.

Ameyazungumza hayo Jana siku ya Jumatatu 24,2023 Katika ukumbi wa Boko chama CCM na kusema kuwa wakina mama wanatakiwa kutokuwa na mambo ya Siri Katika vikundi vyao na kuweza kumkosoa mwezio hadharani na kuweza kumfata kistaarabu na kumwambia na kutoweza kutoa mambo ya Siri ya vikundi vyao na kuyaeka mfukoni na wajifanya hivyo wataendelea.

“Mtu kama anahitaji kujua jambo muelekeze kuliko kutoweza kumuelekeza kwani ukimtengeneza mmoja basi umewatengeneza wanawake 100″Amesema Akbal

Pia amewaomba mkurugenzi wa Buta namkurugenzi wa CRDB wapange Kwa yule ambae wanaitaji kujiunga na menu ya imbeyu wa wape elimu kwa ajili kadi hiyo na kupata mafanikio na kadi hiyo.

Aidha ameweza kuwachangia wanawake hao viti kumi Ili kuweza kujiendeleza Katika vikundi hivyo

Nae mkurugenzi wa Buta Vicoba Endelevu Semeni Mgama amesema wanawake wanafursa 72 ambazo zinazomuhusu mwanamke kwani mwanamke anaouwezo wa kupata mtaji wa laki 2 na ukarudisha hivyo ndani ya mwaka bila riba.

“Kinachotufanya tusifanikiwe wakina mama kutokuwa pamoja na umoja Ili tufanikiwe tuwe Wenye kutoa tofauti zetu na kuacha ubinafsi na maneno maneno madogo madogo”. Amesema Mgama

Madina Mohammed

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram