229 views 2 mins 0 comments

SINEMA ZETU KUTAMBULISHA TAMTHILIA MBILI MPYA

In BURUDANI
July 25, 2023

Azam TV vinara wa huduma bora za maudhui na burudani za kusisimua nchini, kwa mara nyingine wanajivunia kutangaza uzinduzi wa tamthilia mbili zilizokuwa zikisubiriwa kwa muda mrefu zinazoitwa ‘Mtaa wa Kazamoyo’ na ‘Lolita’.

Tamthilia hizi zilizobeba simulizi za kuvutia si tu kwamba zinakuja kuleta mapinduzi ya tasnia ya tamthilia nchini, bali zinaakisi maisha halisi ya Watanzania wa rika zote na zinahusisha waigizaji wenye vipaji na viwango vya juu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katika ukumbi wa hayyat regency Leo jumanne 25 julai amesema Uzalishaji wa tamthilia hizi mbili Mtaa wa Kazamoyo na Lolita umezingatia mahitaji ya soko kwani umetumia vifaa vya uzalishaji vya kisasa na ubora wa hali ya juu wenye uwezo wa kutoa kazi katika viwango vya picha zenye ubora na angavu yaani HD (High Definition).

“Lengo letu la kufanya mambo yote haya ni kuendeleza dhamira yetu ya kutoa burudani ya hali ya juu kwa watazamaji wetu”.

“Mtaa wa Kazamoyo na Lolita zimesanifiwa kwa uangalifu mkubwa ili kuwapa watazamaji aina mbalimbali za simulizi za hadithi zenye kulinda maadili ya Kitanzania, kutoa elimu kwa jamii na zinazotazamika na familia yote. Kwa ufupi tunajivunia kuwa tumetimiza majukumu yetu yote matatu ya msingi yaani tumehabarisha, tumeburudisha na kuelimisha jamii”. Amesema Mganza


Mtaa wa Kazamoyo na Lolita zimetayarishwa kwa ustadi mkubwa zikishirikisha waigizaji mahiri, waandishi wenye ujuzi na watayarishaji wazoefu. Tamthilia hizi zinajumuisha viwango vya juu vya uzalishaji na mbinu za hali ya juu ili kuhakikisha utazamaji wa kuvutia kwa hadhira.

Mtaa wa Kazamoyo na Lolita zitaonyeshwa kwa mara ya kwanza tarehe 4 na 14, Agosti 2023 katika Chaneli ya Sinema Zetu (Chaneli 103) pekee.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram