150 views 41 secs 0 comments

JKCI KUFANYA UPASUAJI WA MKUBWA WA MOYO BILA KUPASUA KIFUA.

In KITAIFA
July 20, 2023

Mwaka wa fedha uliopita wa 2022/2023 Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ilitengewa kiasi cha shilingi Bilioni 44.5 fedha ambazo zimetumika kufanya shughuli mbalimbali za utoaji wa huduma ya matibabu ya moyo Pamoja na shughuli za maendeleo.

 Katika mwaka huo wa fedha  Taasisi imefanikiwa kuwafanyia wagonjwa upasuaji mkubwa wa moyo wakufungua kifua na kuwabadilishia Valvu za moyo moja hadi tatu, upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu  ya moyo (Coronary Artery Bypass Graft Surgery- CABG) Upasuaji wa mishipa yad amu na mapafu walikuwa 714 kati ya hao watu wazima walikuwa 412 na watoto 305.  

Watoto waliofanyiwa upasuaji walikuwa na matatizo ya moyo ya kuziba nayo ambayo ni matundu na mishipa yad amu ya moyo kutokukaa katika mpangilio wake na matatizo ya Valvu.

Kupitia mitambo ya Cathlab (Catherization Laboratory) ambayo ni maabala ya uchunguzi wa matatizo ya tiba ya magonjwa ya moyo inayotumia mionzi maalumu, wagonjwa 2046 kati yao watu wazima 1762 na watoto 284 walipata huduma za matibabu.

Wagonjwa hawa walipata huduma za uchunguzi , matibabu mfumo wa umeme wa moyo, matibabu ya mishipa ya damu  ya moyo iliyokuwa imeziba na kuwawekea vifaa visaidizi vya moyo. Uchunguzi huu Pamoja na tiba unafanyika kwa njia ya upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja.

Editor / Published posts: 21

Journalist

Twitter
Facebook
Youtube
Linkedin
Instagram