114 views 3 mins 0 comments

WAZIRI BITEKO: SERIKALI ITAANZA UTAFITI WA MADINI KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI

In KITAIFA
July 19, 2023

Waziri wa madini Dotto Bitteko Leo amekutana na wanaChama wa Chama cha wachimbaji wa Madini na Wadau mbalimbali wasekta hiyo na kujadili Mafanikio na changamoto za wachimbaji wa madini jijini Dar es Es Salaam

Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es salaam Katika hotel ya Johar rontana na kuhudhuriwa na Waziri wa Maji ,Nishati na Madini Zanzibar, Shaibu Kaduwara na Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Shabani Othman.

Akizungumza na waandishi wa habari waziri dotto biteko amesema serikali imeamua Kwa makusudi Katika mwaka huu wafedha Jinsi watafanya utafiti kwa mara ya kwanza utafiti wa kina kushirikiana na sekta binafsi.

Amesema kutoa Leseni na Leseni itolewe Kwa wote na wasiangalie kundi Moja la wakubwa ukawapa nguvu kubwa ukawaacha wachimbaji wadogo ambao wapo wengi kwasababu wote lazima wachangie.

Aidha pia amesema wanaitaji kupeleka miundombinu kurahisisha biashara Katika sekta ya barabara,maji,umeme na mazingira ya kukodi huwezi kuwageuza wafanyabiashara ambao wanakuletea mtaji Katika nchi yako mukageuka kuwa maadui lazima kuwafanya kuwa marafiki

“Kwa Kasi ambayo Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan anayo Katika sekta ya madini lengo alilowekewa na dira ya maendeleo na ilani ya uchaguzi imetufikisha asilimia 10 Katika DDP teali Mhe.Rais Samia ameshafikisha zote ambazo tulizozifanya hesabu yote ya mwaka wa fedha uliopita ameshafikisha asilimia 9.1 Kwa mwaka huu ni asilimia 9.7 tumefanya wastani wa mwaka mzima tumeshafikisha asilimia 9.1 amekusudia Kwa mwaka 2025 kufikisha asilimia 10”

“Mipango iliyopo na miradi inayoendelea Mhe.Rais Samia itakapofika 2025 atakuja Kwa watanzania kuwaambia kazi aliyotumwa kufikisha sekta ya madini kwenye asilimia 10 itafika Zaidi ya asilimia 10 Kwa sababu mipango ipo na mazingira imekuwa rafiki Zaidi na uzalishaji unaongezeka”. Amesema Biteko

Nae mkurugenzi wa kampuni ya Tembo Nikel Bw.Benedict Busunzu amesema tumeweze kuonyesha mradi wetu ambao umefikia kwenye hatua nzuri kitu kikubwa Katika mradi wetu tunawadau watatu ambao wanatuwezesha mpaka sekta ya madini kufikia hapa na Moja ya wadau wetu ameweza kuweka status Katika soko kubwa la kimataifa la newyork Ili kuweza kupata kepito Katika soko hilo la marekani.

“Katika upande wa Tembo Nikel Katika upande wa kukusanya fedha Kwa ajili ya kuanzisha mradi wetu tunaamini kwamba tunauwezo Sasa tunanjia sahihi ya kuweza kukusanya fedha Kwa ajili ya kuweza kuanzisha mradi wetu”.

“Katika mradi wetu wa madini fedha ni kitu muhimu Zaidi Kwa sababu wachimbaji au waazishaji wa mradi wapo kila sehemu Kwa hiyo teali tumeshasetiwa swala la fedha tunauwakika Sasa mpango tuliojiwekea kwamba miradi yetu uanze ujenzi na kuweza kuhakikisha tunaweza kuzalisha madini yetu ya Nikel Kwa mara ya kwanza tunategemea mwaka 2026 tutakuwana madini yetu ya Nikel tutakayoanzishwa hapa Tanzania”. Amesema Busunzu

Madina Mohammed

/ Published posts: 1205

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram