MWENYEKITI wa zamani wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salum amefariki dunia leo.
Taarifa zinaeleza Jecha Salum amefariki akiwa katika Hospitali ya Lugalo Dar es Salaam.
Maziko yanatarajiwa kufanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja Visiwani Zanzibar.
Ikumbukwe mwenyekiti huyo aliwahi kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Mwaka 2020, Jecha alichukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).