
Mkutano wa umoja wa Askari wa kike Duniani (IAWP) Kanda ya Afrika unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Julai 22-29-2023 unaotarajiwa kuongeza uhusiano baina ya Askari wa kike wa Tanzania na Askari wa nchi nyingine ambazo zitashiriki.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF-Net) Kamishna wa Polisi CP Suzan Kaganda amesema hayo leo baada ya kumalizika kwa Matembezi ya KM 5 Jijjni Dodoma yakihusisha Maofisa, Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali, Wasimamizi wa Sheria na Wadau mbalimbali ikiwa ni uhamasishaji kuelekea Mkutano huo.

Wananchi wote wamekaribishwa kuhudhuria ufunguzi utakaofanyika Julai 23, 2023 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.