450 views 34 secs 0 comments

RAIS SAMIA:APOKEA TAARIFA RASMI YA TUME YA HAKI JINAI

In KITAIFA
July 15, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amezitaka taasisi za haki jinai kufanya marekebisho ambayo hayana gharama za kifedha katika mifumo yao ya kiutendaji ili kuleta haki kwa wananchi.


Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akipokea taarifa rasmi ya Tume ya Kuangalia jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai hapa nchini katika hafla
iliyofanyika Ikulu.


Aidha, Rais Samia amesema ni vyema marekebisho hayo yafanyike kabla ya
mabadiliko ya kiutawala na kiufundi yanayoigharimu serikali fedha nyingi.
Rais Samia pia ameelekeza kufanyiwe kazi masuala ya kuheshimu watuhumiwa
kwenye ukamataji, upelelezi pamoja na uendeshaji wa mashtaka mbalimbali ili haki iweze kutendeka.


Vile vile, Rais Samia amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama visitoe kipaumbele
katika kukamata na kuhukumu na badala yake vijikite kuzuia kutenda makosa.

Kwa upande mwingine Rais Samia amevitaka vyombo vya jinai kuwa na mfumo unaosomana katika uendeshaji ili kurahisisha ufuatiliaji pamoja na kuzuia mfumo wa upelelezi kutoa mwanya wa rushwa.


Tume ya Haki Jinai iliyoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman ilikusanya maoni kutoka taasisi 12 kwa lengo la kupata ushauri na mapendekezo ya namna bora ya kuimarisha mfumo na utendaji kazi wa taasisi zinazohusika na haki jinai.

/ Published posts: 1615

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram