UNAPOPENDWA,ukapendeka na upande ukapendwa,furaha,utulivu na amani huwa ni rafiki zako wa karibu.
Wataalam wa Masuala ya mahusiano wanasema Katika upendo huu, mwanamke ndiye anaouwezo Zaidi WA kupenda kuliko mwanaume,kwamba mwanamke akipenda anapenda Hadi anazubaa.
Kwa upande wa mwanaume huwa anapenda Kwa hesabu ni nadra sana kumpata mwanaume akazama kwenye mapenzi kiasi kwamba anazubaa na kuduwaa na kuchanganyikiwa
Wengi huwa wanatanguliza majukumu na ndio maana sio vigumu Kwa akina kaka kuwa na mwanamke Zaidi ya mmoja akaweza kuwahudumia na kuwamudu wote Kwa pamoja.
Ni tofauti kidogo Kwa mwanamke kwani ni wachache sana waliojaliwa kipajicha kuwa na wanaume wengi Kwa wakati mmoja na kuweza kuwaridhisha wote Kwa pamoja.
Na ndiyo maana sio vigumu sana kugundua mwanamke anapoanza usaliti,kwani uwezo wa hadaa ya mapenzi sio makubwa kiasi Cha kuficha hisia walizo nazo.
Mwanamke akifanya mapenzi na akaridhika vizuri.ana uwezo wa kuonyesha upendo na asitamani mwanaume mwingine Hadi pale atakapoona upendo na mapenzi yanapungua.
Mwanaume anahitaji Zaidi heshima na utii kutoka Kwa mwanamke na sio tu kurushwa roho kutamfanya asisaliti,lakini wanamke waliowengi huganda Katika mahusiano kwasababu ya kuridhika na tendo la ndoa Zaidi ya vitu viรฑgine.
Mwanamke akifanya mapenzi akaridhika, anaouwezo wa kukaa bila ya tamaa ya kufanya tendo la ndoa hata Zaidi ya miezi minne ikiwa Yuko mbali na kishawishi au mpenzi wake,lakini mwanaume anaouwezo wa kufanya mapenzi hata Zaidi ya mara tano Kwa siku na mwanamke mmoja au wanawake tofauti.
Wanaume ana uwezo wa kumaliza kufanya tendo la ndoa na kupoteza hisia Kwa kiwango kikubwa sana kuliko mwanamke ambaye ubongo wake una uwezo wa kutunza kila aina ya hatua Katika tendo la ndoa.
Hivyo hali halisi ni kwamba mwanaume hatekwi na mapenzi Kwa sababu ya kurushwa roho mfululizo Bali hufurahia Zaidi kuheshimiwa na kutambuliwa jukumu lake la kutimiza mahitaji ya mwezake amafamilia
Baadhi ya akina kaka wanadhani kumwambia kuwa mwanamke unampenda kunamaliza kila kitu Katika mahusiano,bila ya kujua kuwa unapoamua kumshirikisha Katika maisha yako kunamfanya akuamini na akupende Zaidi
Mรกsuala ya pesa yanachukua nafasi kubwa,Kwa mwanamke anaekupenda na anataka kufika mbali nawe kawaida anakuwa muoga kukuomba hela kama Yuko na shida hawezi kuwa mwepesi WA kutaja kuwa anataka pesa na hata kama anataka hawezi kusema kiwango Cha juu kama ambavyo ingekuwa Kwa mwanamke ambaye Yuko na mwanaume Kwa sababu ya maslahi yake binafsi.
Madina Mohammed