328 views 5 mins 0 comments

WAZIRI MBARAWA:AKATA MZIZI WA FITINA

In KITAIFA
July 14, 2023

Waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof.makame mbalawa amesema Tarehe 10 juni mwaka huu Bunge la yamhuri ya Muungano wa Tanzania lililidhia Azimio la makubaliano kati ya serikali ya Muungano Tanzania na serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi wa kijamii kwa ajili ya Utekelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari Tanzania pamoja na kuridhiwa huko na bunge letu tukufu serikali imeona kuwa Kuna umuhimu mkubwa sana wa kuendelea kutoa elimu Kwa wadau mbalimbali ambao tulianza Kwa viongozi wetu wa dini na wafanyakazi wa mamlaka ya bandari Tanzania pamoja na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari hapa Nchini jijini dar es salaam Katika ukumbi wa hayyat regency Leo (ijumaa14 julai 2023) Amesema mamlaka ya Usimamizi wa bandari Tanzania TPA ilianzishwa Kupitia Sheria namba 17 ya mwaka 2004,mamlaka hiyo ilirithi na kuchukua majukumu yaliyokuwa mamlaka ya bandari ya Tanzania iliyoanzishwa kupitia Sheria namba 12 ya mwaka 1977 baada ya kuvunjika Kwa iliyokuwa jumuiya ya Africa mashariki.

Amesema madhumuni makubwa ya kuanzishwa Kwa TPA ni kuhakikisha nchi yetu inaendelea kunufaika na faida ya kijigografia kutokana na usafirishaji wa mizigo na abiria kupitia sekta ya usafiri au usafirishaji wa majini.

“Kwa ujumla serikali zetu Kwa awamu mbalimbali zimeendelea kuwekeza kwenye bandari zetu Kwa vipindi tofauti tofauti kwa kutumia fedha kutoka vyanzo vyake vya ndani na fedha za mikopo Kwa lengo la kuboresha sekta ya bandari nchini pamoja na serikali kuchukua juhudi mbalimbali za maboresho ya bandari zetu Bado ufanisi Katika utoaji wa huduma za kibandari haujafikiwa viwango vinavyotakiwa kimataifa”.Amesema waziri mbarawa

Aidha hali ya ufanisi wa bandari ya Dar es salaam na bandari nyingine zinazoendeshwa Moja Kwa Moja na mamlaka ya bandari Tanzania huko chini sana udhaifu huu unaonekana waziwazi kwenye utendaji wa kila siku wa bandari zetu pamoja na ukusanyaji wa mapato Kwa ujumla bandari zetu hasa bandari ya Dar es salaam haifanyi vizuri na inaendelea kuwa kwenye kiwango Cha chini Katika utendaji ukilinganisha na bandari shindani kikanda.

“Wastani wa meli kusubiri nangani kwa bandari ya Dar es salaam ni siku 5 ambayo sawa na masaa 120 ikilinganishwa na siku Moja Kwa masaa 6 Kwa bandari ya Mombasa ambayo ni masaa 30 na siku 1 inamasaa 15 ambayo sawa na masaa 39 Kwa bandari ya Dabani huko African kusini meli inatumika mda mrefu kupAkia na kupakua shehena gatini Kwa wastani wa siku 3 ikilinganishwa na siku 1 inayokubalika kimataifa”.amesema waziri mbarawa

Changamoto ambazo zinazokosekana nikama zifuatazo 1. kukosekana na mifumo ya kisasa ya Tehama 2.kutokuwepo Kwa maeneo ya kutosha ndani na nje ya bandari ya kuhifadhia shehena za mizigo pamoja na maegesho ya kutosha ya kuegeshea meli 3.kukosekana mitambo ya kutosha ya kisasa kuhudumia shehena ambayo inabadilika mara Kwa mara Kwa kubadilika teknolojia mpya ambayo inagharama kubwa za uwekezaji.

Hata hivyo Amesisitiza kuwa Muda wa kuondoshaji mizigo Kwa bandari ya Dar es salaam kuwa mkubwa takribani masaa 12 ikilinganishwa na bandari nyingine, ufanisi huo mdogo wa bandari ya Dar es salaam inatokana na changamoto mbalimbali

Athari za kutokuwa na ufanisi Katika bandari ya Dar es salaam ni pamoja na meli kusubiri Muda mrefu kunasababisha kuongezeka Kwa gharama Kwa kutumia bandari ya Dar es salaam Kwa mfano gharama za meli kusubili nangani Kwa siku Moja ni takribani Dola za kimarekani elfu 25 sawa na pesa za kitanzania milioni 58

Meli kutumia Muda mrefu kupAkia na kupakua shehena Kwa wastani wa siku 5 ikilinganishwa na siku 1 inayokubalika kimataifa

Meli kubwa Kwa kutokuja Katika bandari ya Dar es salaam kutokana Kwa kuchukua Muda mrefu WA kuhudumia na hivyo kusababisha bandari yetu kuripoti na kuongeza gharama Kwa kutumia bandari ya Dar es salaam Kwa mfano Kwa Sasa meli zinazohudumiwa na bandari ya Dar es salaam zinauwezo WA kubeba au kuingiza meli zenye uwezo WA kubeba makasha

Kati ya elfu 2400 mpaka 2800 meli kama hizi zinachukua takribani siku 5 au 6 bandari za nchi jirani zinauwezo wa kubeba makasha elfu 4 meli zinazokuja hapa zinabeba makasha elfu 2800

Madina Mohammed

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram