Sakata la bandari likiwa linazidi kuendelea viongozi mbalimbali, wanasheria,pia wanaharakati wanazidi kuliongelea swala hilo la bandari na kuzidi kutoa ufafanuzi wa kina Ili wananchi waelewe kuwa bandari haiuzwi Bali ni uwekezaji ambao utakuwepo baina ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai.
Wahariri mbalimbali nao wameweza kutoa maoni Yao wakilizungumzia swala hilo Ili kuwaelimisha jamii Kwa kina kuhusiana na bandari kuwa unekezaji uliofanywa ni uwekezaji sahihi na Wala hautoweza kupata madhara Katika uwekezaji huu.
Joseph mwendapole ni mwanachama wa Jimbo la wahariri TEFF amesema Mhe.Waziri mbarawa Kwa kweli amefafanua ukiangalia Katika hutuba ambayo ameitoa Leo Haina tofauti na Ile ambayo alieitoa Bungeni amefafanua maslahi ya taifa yatokayo Kwa kuzingatia kwenye makubaliano ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai na mambo mengi yalizungumzwa wakati ule ameyarudia tena Katika hutuba yake ya Leo.
“Amefafanua Kwa mfano Ajira za Tanzania za pale bandarini amesema jamani pale wapo watu elfu 20 wakija wale waliowekeza Ajira zitaongezeka elfu 71 na maswala ya ardhi kwani wale watu wakija kuwekeza DP WORLD haitatawaliwa Wala haitauzwa kwao ardhi itakodishwa na mtu akikodishwa kwahiyo huwezi kuwa yako”.
“amefafanua kuhusu maswala ya usalama kwamba usalama itabaki kuwa jukumu la serikali amezungumzia kuhusu kodi watu wanamaswali kuhusu kodi kuwa watakuwa wanakusanya kodi amesema mamlaka ya mapato Tanzania TPA itaendelea kukusanya kodi kama kawaida kwahiyo mapato yataongezeka Kwa Sababu Kwa Sasa TRA wanakusanya Trillion 7 lakini endapo watakuja wale ufanisi utaongezeka mizigo ya nchi jirani itapitia mingi Tanzania TRA itakusanya Zaidi ya Trillion 20 Kwa mwaka”. amesema mwendapole
Aidha amesema maslahi ya taifa yamezungumzwa Kwa kirefu sana kama tutaelewa huu uwekezaji ni mzuri ambao utakaokuza uchumi wetu.
Madina Mohammed