195 views 3 mins 0 comments

UBONGO KIDS WAADHIMISHA MIAKA 10

In KITAIFA
July 13, 2023

Ubongo Kids yasherehekea miaka kumi tangu kuanzishwa kwake ikiwa na mafanikio makubwa ya kuenea nchi 23 na kuzifikia familia milioni 32 kote duniani.

Ubongo Kids ambayo imekuwa kinara hapa nchini kutokana na umahili wa kuandaa maudhui ya kuelimisha na kuburudisha kwa vipindi kwenye televisheni wamesherekea mafanikio hayo kwa kuzindua silizi mpya ya NUZO na NAMI Ili kuwaburudisha watoto

UBUNGO KIDS walikuwa wanapambana Kwa kila njia Ili maradi watoto waweze kufurahi na kuelimika na kujifunza Kwa kupitia katuni za vitendo tena hasa Kwa wale wenye tatizo la kutoshika kitu mapema Kwa kuwaelimisha kwenye hisabati na Kiingereza.

Akizungumza na waandishi jijini dar es salaam Katika ukumbi wa mlimani city Leo (Alhamis 13 julai 2023)Mmoja wa waanzilishi wa ubongo Bw.Rajabu Semtawa amesema wazo lilikuwa limeanza kipindi hicho katuni nyingi watoto wengi walikuwa wanapenda kuangalia katuni za nje Sasa sisi tukafikiria tukasema je? Watoto wanapenda sana katuni sisi tukaona hatuna katuni za kitanzania ambazo wahusika wanaongea Kwa kiswahili.

“kunakuwa na utamaduni wa kuongea kiswahili lakini tumeona vile vile Kuna tatizo la mashuleni ambalo watoto wengi wanaogopa hesabu tukafikiria tunaweza tukatengeneza katuni lakini hizi katuni tunaweza kuingizia na masomo juu yake kwani watoto wanaburudika na Muda huohuo wanaelimika vilevile Kwa hiyo tukaona bola itumike sana hii ya katuni”

“kutengeneza kitu ambacho kitamburudisha mtoto lakini pia kitamuelimisha Kwa wakati huohuo Kwa hilo lilikuwa wazo kubwa sana tunashukuru baada ya kuanzisha hicho kitu tumeona watoto wakawa wanapenda hizo katuni zetu wengine wakawa wanakuja ofisini kwetu wanasema wanataka Zaidi na Zaidi lakini kama unavyojua ndo kitu tulikuwa tumekianza mwanzo Timu ilikuwa Bado ndogo kwahiyo tukaangalia uwezekano WA kuanza kufanya nyingi Zaidi Kwa ajili ya kukidhi haja za watoto Kwa kipindi hicho”.Amesema Semtawa

Aidha Semtawa amesema baada ya hapo tukaangalia Kwa kuanza na watano tukaona Muda sahihi WA kuanza watano tukaona Muda sahihi WA kutengeneza Timu ambayo tutakayoweza kutengeneza content nyingi Zaidi Kwa ajili kuwafikia watoto na kuwaelimisha Zaidi.

Nae Maisala Mohammed alimaarufu Kama Mai zumo ni mchekeshaji na pia ni muigizaji wa movie mbalimbali ambae Katika taasisi hii ya ubongo kids alikuwa Moja ya memba wa kutafsiri video za AKILI ME na UBONGO KIDS amesema video hizo ambazo zinawasaidia watoto kielimu,kujitambua,kujisaidia,na pia Wenye wanapopata changamoto mbalimbali na kwa Sasa tumewaletea silizi mpya iitwayo NUZO na NAMI ambayo tulishawai kuifanyia uzinduzi wake hapa hapa mlimani city.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1886

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram