
Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya double Eight LTD Marshalo V. Chikoleka Amesema swala la bandari limebeba uchumi wa nchi yetu ya Tanzania ni sehemu ambayo inayoonyesha Kwa miaka yote ni sehemu ambayo ni maarum inayobeba uchumi wetu Kwa kiasi kikubwa sana.
Akiyazungumza hayo jijini dar es salaam Leo (jumanne 11 julai 2023) amesema bandari ni Moja wapo ya uchumi na inashughuli mbalimbali ambazo jamii zetu za kitanzania zinapata mapato yake kutokana na bandari na nchi yenyewe Kwa ujumla inapata faida mbalimbali ya mapato kutoka bandarini.
“kutokana na uwekezaji ambao uliokuja Sasa hivi huu wa Dp World ni uwekezaji ambao watanzania tunaupenda na tunautaka sana uwepo na hii kutokana na shughuli zetu za bandari ni sehemu ambayo ni nyeti ya kitaifa ambayo shughuli mbalimbali za hapa na pale zinafanyika”.
“Kwa hiyo hili swala sio swala la kichama Wala sio swala la mtu binafsi na sio swala la kisiasa bali hili swala ni la kitaifa na mwenendo wake inabidi twende kitaifa na sio Kwa kuwavuta watu baadhi wa chama na wanasiasa na watu binafsi”. Amesema Chikoleka
Aidha Amesisitiza swala hili limakaa kisheria Zaidi na taifa letu Kuna wasomi wa kisheria wanajitahidi sana kutuelimisha na kutuelekeza kuhusiana na mkataba huu Jinsia ulivyo Kwa kuongelea madhara ya mkataba na faida yake wameuchambua kwa undani Zaidi Ili kutoa elimu Kwa jamii juu ya Tanzania Katika kuonyesha madhara yake na faida yake na wengine wameenda mbali Zaidi Hadi wameenda mahakamani kwenda kuupinga mkataba huu usiweze kusonga mbele.
Hata hivyo ameweza kusifia kuwa Kuna wanasheria ambao wameshajitokeza kama Prof.Shivj ameuelezea mkataba kiundani na kusema madhara yake na faida yake juu ya mkataba huu na akauchambua vizuri.
Pia ametoa wito kuwa maoni hayo ambayo yaliyoweza kutolewa na wanasheria mbalimbali yaweze kusikilizwa na kuangaliwa weakness zilizokuwa Katika mkataba,pia tunaweza kuwatumia hawa wanasheria Kwa kuangalia Jinsia Gani Kwa kuweza kurudi nyuma na kuangalia tunaweza kurekebisha wapi Kwa kuweza kupata kitu kizuri Kwa faida ya Vijana wetu.
Madina Mohammed