Ripoti mpya ya FinScope Tanzania 2023, ambayo ni ya awamu ya tano imezinduliwa Leo Jijini Dar es salaam,ambao utafiti Huo unaangazia hupima mahitaji,upatikanaji na matumizi ya huduma za fedha Tanzania Bara na Visiwani.
Ripoti hiyo imezinduliwa Leo Jumatatu ya tarehe 10 Katika ukumbi WA BOT Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Natu Mwamba naGavana wa Benki Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ujumuishaji wa Huduma za Fedha, Bw. Emmanuel Tutuba.
Utafiti uliozinduliwa mwaka huu ni mwendelezo wa tafiti zilizofanyika miaka ya 2006, 2009, 2013 na 2017, ambazo zililenga kufuatilia na kulinganisha mifumo yote ya matumizi ya huduma rasmi za fedha na zisizo rasmi kwa takriban miongo miwili.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu Wizara ya fedha na mipango Dkt.Natu Mwamba Amesema Nimeridhishwa kuona ripoti ikionyesha kwamba ujumuishaji wa huduma rasmi za fedha umeimarika kwa kiasi kikubwa
tangu utafiti wa mwisho uliofanyika mwaka 2017, ambapo ripoti imeonyesha ufanisi umeongezeka kutoka asilimia 65 hadi asilimia 76 . Pia kwamba tofauti ya uwiano wa ujumuishaji wa huduma za fedha baina za jinsia zote umepungua kwa kiwango kikubwa.
“bado kuna kudorora kwa pengo jinsia katika ujumuishi wa huduma zinazotolewa na mabenki”, ambapo aliitaja kuwa ni fursa kubwa kwa wawakirishi wa taasisi za kibenki”. amesema Mwamba
Hata hivyo Mwamba Amesema Tofauti na sekta nyingine ndogo, uenezaji wa huduma za bima umepungua (kutoka asilimia 15 hadi 10), hali ambayo pia ni kinyume na lengo la Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha, ambao unakusudia kufikia asilimia 50 ya watu wazima kupata na kutumia huduma za bima ifikapo 2023.
“Juhudi madhubuti zinahitajika kwa watunga sera, wadhibiti pamoja na watoa huduma za fedha na wabunifu ili kukabiliana na changamoto za sekta kwa upana wake kwa kutoa bidhaa mpya zitakazokidhi mahitaji ya Watanzania ya kupunguza athari zinazoweza kujitokeza”. Amesema Mwamba
Nae Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amesisitiza
zaidi juu ya umuhimu wa tafiti kama FinScope Tanzania kwa ajili ya kuendelea kupima hali ya ujumuishwaji katika huduma ya kifedha, na umuhimu wake katika upimaji na uundaji wa Mpango wa Taifa ya Ujumuishwaji wa Huduma za Fedha kwa ujumla.
Aidha aliwahakikishia wajumbe hao kuwa mwelekeo ulioonyeshwa na FinScope Tanzania 2023,hususani mapungufu, ambayo yameonyesha wazi hitaji kubwa la matumizi ya mara kwa mara ili kuongeza ukuaji wa fedha, utaarifu mabadiliko muhimu katika Mpango mpya wa Ujumuishwaji wa Huduma za Fedha wa 2023-2026, ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT) Bw.Eric Massinda amesema Uzinduzi wa ripoti ya matokeo haya muhimu ni mwanzo tu wa ushirikishaji mkubwa wa sekta ya umma katika harakati za kuiwezesha sekta kufanya maamuzi kutokana na Ushahidi wa kina na uundaji wa bidhaa katika sekta ya fedha
Amesema kutakuwa na ushirikishaji na mazungumzo ya kina na wadau kwa ajili ya kupanua wigo wa usambazaji wa matokeo ya FinScope Tanzania 2023 kwa kipindi cha miezi kadhaa ijayo.
Kuhusu ripoti ya FinScope Tanzania 2023
FinScope Tanzania ni utafiti wa kina wa mahitaji ya sekta ya kifedha kwa watu wazima wa Kitanzania wenye umri wa kuanzia miaka 16 na kuendelea.
Ripoti hii inatoa ufahamu wa hali ya matumizi ya huduma za kifedha nchini kote na ni kipimo cha kuaminika kwa mahitaji na matumizi ya huduma za kifedha katika makundi mbalimbali ya watu.
Madina Mohammed