Kufuatia Kwa kutungwa Kwa Sheria ya mipango ya taifa ya mwaka 2023 pamoja na uamuzi WA kuhamishia Masuala ya uwekezaji Ofisi ya Rais.Hivyo,Rais WA Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya miundo ya wizara na kufanya uteuzi WA viongozi Kama ifuatavyo.
Mhe.Rais Samia Suluhu ameunda Ofisi ya Rais,mipango na uwekezaji ambapo amemteuwa Profesa Kitila Elexander Mkumbo kuwa waziri wa nchi.Ofisi ya Rais mipango na uwekezaji Mhe.prof Mkumbo ni Mbunge wa Jimbo la ubungo.
Pia ameunda wizara ya fedha ambapo amemteuwa Mhe. Dkt mwigulu Nchemba alikuwa waziri wa fedha na mipango.
Hata hivyo ameunda wizara ya viwanda na biashara ambapo amemteuwa Mhe.Dkt Ashantu Kachwamba kijaji kuwa waziri wa wizara hiyo,kabla ya uteuzi huo Mhe.Dkt kijaji alikuwa waziri wa uwekezaji,viwanda na biashara.
Pia Amemteuwa Bw.Lawrence Nyansebwa mafuru kuwa katibu mtendaji WA tume ya mipango ya taifa,kabla ya uteuzi huo Bw.mafuru Naibu katibu mkuu Wizara ya fedha na mipango (usimamizi wa uchumi)
Amemteuwa Bw.Elijah mwandumbya kuwa naibu katibu mkuu, Wizara ya fedha (Usimamizi wa uchumi) kabla ya uteuzi huo Bw.mwandumbya alikuwa kamishna idara ya uchambuzi wa sera wizara ya fedha na mipango.