99 views 3 mins 0 comments

MINGLE FC KUICHAPA TING WAYLAND KWENYE KATA YAO

In MICHEZO
July 03, 2023

Mashindano Kimwanga CUP ambayo yalikuwa yakitimuwa vumbi kata ya Makurumla yametamatika siku ya jana baada ya Timu ya Mingle FC kunyakuwa kikombe kwa kuichapa Ting Wayland Magoli mawili kwa sifuri mchezo uliochezwa uwanja wa Bubu.

Katika fainali ya michuano hiyo iliyoteka hisia za mashabiki lukuki wa soka katika Kata ya Makurumla pamoja na kata jirani zilizopo katika jimbo la Ubungo mbali ya kujitokeza mamia ya wananchi kushuhudia mtanange wa timu hizo zilizotinga fainali, mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Abass Mtemvu.

Mchezo wa fainali ya mashindano ya Kimwanga CUP, ulitanguliwa na mchezo wa Rede ulioandaliwa na Diwani wa Viti Maalum, Hawa Abdulrahman ambapo mshindi katika fainali hizo naye alinyakua ng’ombe na wa pili mbuzi, ambapo michezo hiyo ilifanyika katika Uwanja Bubu ulioko Mtaa wa Kwa Jongo Kata ya Makurumla ambapo wananchi wameshuhudia ushindani mkali kutoka kwa timu hizo ambazo ziliingia fainali huku kila mmoja akiwa na ndoto ya kutaka kuchukua Ng’ombe.

Lakini hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika Mingle FC wakaibuka washindi na hivyo kukabidhiwa zawadi zao kama ambavyo ziliahidiwa na Diwani Kimwanga.

Akizungumza kwenye fainali hizo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abass Mtemvu amesema kupitia mashindano ya Kimwanga CUP wao kama Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam wamejiridhisha kazi inakwenda vizuri huku akihamasisha madiwani wengine kuiga mfano huo na kwamba mashindano hayo yawe chachu kwa madiwani ambao hawajaanzisha sasa waanzishe mashindano kama njia ya kukutana na watu na kuwa karibu nao.

Pia Mbunge wa Jimbo la ubungo professor kitila mkumbo amekabidhi pesa taslim laki mbili Kwa wachezaji wa mpira wa miguu ambao kwa kila mmoja amepata laki timu ya wailend na timu ya Mingo FC

Timu hizo mbili zilifika finali na kufungana magoli 2-0,Timu ya mingo ndo iliyoweza kuchukua ubingwa huo Kwa kuwafunga Ting Wayland bao 2 kwa sifuli.

Ting Wayland wameshindwa kuchukua ubingwa huo Katika mtaa wao wa kimamba na kuzidiwa uwezo na watoto WA mingle FC wa mtaa wa kilimahewa

Kwa mshindi wa kwanza amepata kikombe na ng’ombe mmoja na pesa laki moja na mshindi wa pili amepata mbuzi mmoja na pesa laki mmoja kutoka kwa mbunge Profesa Kitila Mkumbo

Aidha mgeni rasmi ambae pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu amewapa Seti moja moja kwa kila Timu na mipira miwili kila timu.

Awali Diwani wa Kata ya Makurumla Bakari Kimwanga amemshukuru Mungu kwa mashindano hayo kufika hatua ya fainali na kukabidhi zawadi kama alivyoahidi na tangu kuanza kwa michuano hiyo wamepita kwenye milima na mabonde na kila ilipojitokeza changamoto waliitatua kwa wakati.

Michuano hiyo ilianza mwezi wa 3 na kuzinduliwa na Mheshimiwa Mbunge Profesa Kitila Mkumbo na kufikia tamati siku ya jana.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram