523 views 29 secs 0 comments

KUKANUSHA TANGAZO LINALOSAMBAA KWENYE MITANDAO KUHUSU
MPANGO WA RAIS WA UWEZESHAJI WA VIJANA

In KITAIFA
July 01, 2023


Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa za utapeli zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa Mpango wa Rais wa Uwezeshaji wa Vijana, Taarifa hiyo yenye kichwa cha habari “Mpango wa Rais wa Uwezeshaji Vijana”, inawahamasisha Vijana kuomba Ufadhili wa kitaifa wa uwezeshaji vijana 2023 kupitia Tovuti yenye anuani;(https://youth.empower.tzn.formsite.online) kwa ajili ya zoezi la Usajili ili waweze kuwezeshwa katika shughuli zao za Biashara.


Elimu Umma unajulishwa kuwa hakuna mpango huo unaotajwa na kwamba taarifa inayosambazwa kupitia mitandao ya kijamii si ya kweli na inalenga kuwatapeli wananchi.


Serikali inaendelea kutumia fursa hii kuutarifu umma kuwa kwa vijana wote ambao wanahitaji huduma za Uwezeshaji wa mikopo kwaa ajili ya kupata mitaji kwa njia ya mikopo ili kuanzisha au kuendeleza miradi yao ya uzalishaji mali wanaweza kupata taarifa kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (Youth Development Fund-YDF) katika Ofisi na Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu; (www.kazi.go.tz) au katika madawati ya
Maendeleo ya Vijana yaliyo katika Idara za Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri zote 184 za Tanzania bara.

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram