121 views 2 mins 0 comments

Wadau wapewa somo Kwa ajili ya kulipa kodi mataasisi yao

In KITAIFA
June 30, 2023

Mashirika yasiyo ya kiserikali Kwa kushirikiana na serikali wamefanya mkutano maarumu Kwa ajili ya wadau na kuwapa somo wadau hao Kwa ajili ya kulipa kodi na kutatua changamoto mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo ijumaa ya tarehe 30 mwenyekiti WA bodi ya uratibu WA mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania Mwamtumu Mahiza amesema mashirika yasiyo ya kiserikali ni miongoni WA wadau wanaopaswa kulipa kodi za aina mbalimbali na kumekuwepo na changamoto za kiufundi na za kiutaaramu ambazo Kwa pamoja tumeona kupata mkutano waweze kupitishwa na kuelimishwa.

“Kwa pamoja tumefanya majadiliano Ili kodi ziweze kulipika na pale ambapo kunaonekana kunachangamoto basi zinapaswa kuwasilishwa Katika serikali kuu Kwa ajili ya kupata ufumbuzi WA changamoto hizo”.

“Kwanza Kuna ENGO’s zote zimewekwa mahali pamoja Katika ulipwaji WA kodi hali ya kuwa changamoto ni kwamba ENGO’s hizi zinamatabaka zipo za kimataifa,zipo za kitaifa na halafu zipo za kawaida sana Kwa hiyo kazi kubwa kama bodi itabidi tukae tujipange tuone tunawatambulishaje Kwa TRA”.Alisema Mahiza

Aidha Mahiza amesema tunawaomba mkutano mkubwa na viongozi WAkuu WA TRA Ili kuwasilisha maoni ya wadau na Kwa pamoja tutashirikiana kuona changamoto hizi zinatatuliwa na kuleta ufanisi Kwa sababu nafasi ya mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali Kwa jamii ni kubwa sana wanafanya mambo mengi na tusingependa kuwakatisha tamaa

Nae Mratibu wa mtandao wawatetezi Wa haki za binadamu wakili Onesmo olengurumwa amesema ikitokea taasisi imesajiliwa na haijawai kufanya zero litaini maana yake tunaenda kutoa taarifa kuwa hamna pesa utaona kule taasisi imetoa pesa nyingi sana na imepigwa penati nyingi na riba wanazipata kubwa sana.

Hata hivyo Mahiza ameongezea Kwa kusema kuwa tumebaini kwamba mashirika mengi yanaongozwa na Vijana ambao serikali Katika hali ya kawaida wangepaswa kuwapa Ajira lakini wenyewe wamekuwa wabunifu wameweza kuajili na kujiajili na kuwajili Vijana wezao Kwa hili ni jambo la kuwatia moyo Kama sisi serikali tutaketi nao pamoja na tuone tunapangana nao vipi Ili kuleta ufanisi Zaidi.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1212

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram