123 views 2 mins 0 comments

TARO NA KAMATI YA BUNGENI YAWASILISHA MAPENDEKEZO YA WADAU WA SANAA

In BURUDANI
June 30, 2023

Taasisi ya Haki za Wasanii (TARO) wamekutana na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria na kuwasilisha mapendekezo ya wadau wa sanaa juu ya Marekebisho ya Sheria ya Sanaa namba 23 ya mwaka 1984 Ili kuendana na uhuru wa sanaa kama msingi wa haki za binadamu.

Akizungumza Katika kikao hicho Leo ijumaa tarehe 30 Mkurugenzi wa utawala TARO Joshua Msambila amesema wasanii wamekuwa hawana ubunifu wanaogopa kufanya ubunifu kuyafikiria sana na kuyaongelea matatizo Katika jamii mbalimbali na tumeona Kuna vitu mbalimbali Kwa wasanii wanataka kuwasilisha lakini kunachangamoto zinakuwa kubwa Akiwasilisha Ile na napata changamoto kubwa

“Hii Sheria inawajengea hofu wasanii na kudhibiti uhuru WA kutoa maoni pia inavunja haki ya kikatiba ya uhuru WA kutoa maoni sie tunaamini kwamba katiba yetu imelipa haki sisi wasanii kutoa haki ya maoni mbalimbali kuhusu maisha yetu ya kila siku”.Amesema Msambila

Aidha Msambila amesema nchi yetu Haina sera ya Sanaa Kuna nchi ambazo zimefanikiwa Katika sera ya za Sanaa sisi tumefanikiwa kwenye sera ya kiutamaduni ambazo unazungumzia Sanaa kidogo na mchezo kidogo na Sanaa inamambo mengi sana inahitaji kuwa na sera ambayo inatupa muongozo Kwa namba ya kusaidia Sanaa kuweza kukua na kuweka tija mbeleni.

Hata hivyo ameongeza Kwa kusema kuwa pia tumeona Kuna maeneo ya umma na ya waziri kufanyia kazi ya Sanaa yanageuzwa matumizi yake na kujenga majumba ya kibiashara tumeona baadhi ya kumbi Kama DDC iliyopo KARIAKOO na imegeuzwa kuwa bar na kuuzia chakula pia ukumbi mwengine kichangani uliopo morogoro na mnazi mmoja.

Nae Mjumbe WA kamati ya Elimu, Maendeleo na Utamaduni Anastazia Wambura ametoa mchango wake na kusema kwenye mfuko WA Sanaa ukiuangalia Katika tangu za siku ya nyuma huoni kama kunachochote kinachoendiketi Kwa kuzingatia usawa WA Jinsia wakati WA matumizi ya mfuko WA Sanaa bahati mbaya ulipotea ila Sasa hivi umerudi tena.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram