210 views 2 mins 0 comments

Jeshi la polisi linaendeleza kuzuia vitendo vya kiharifu

In KITAIFA
June 29, 2023

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kusimamia mifumo ya kuzuia, kubaini na kupambana na vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari kamanda WA polisi Kanda maarum muliro jumanne muliro amesema Operesheni kali maalum iliyoanza mwezi Aprili, 2023 na inayo endelea katika maeneo mbalimbali
ya Jiji imefanikiwa kuwanasa watuhumiwa sugu 48 wa matukio ya unyangโ€™anyi na uvunjaji nyumba
usiku na kuiba.

“Waliokamatwa ni Michael Jacob ngatunga mwenye miaka 38 mkazi wa Jet lumo,Hossein Rashid mwenye miaka 40 Mkazi wa Mtoni Mtongani na Mussa Mohamedi mwenye miaka 23 mkazi wa Chanika, na wote ni wakazi wa Dar es Salaam”Alisema muliro


Watuhumiwa hao wamekamatwa na vitu mbalimbali walivyoiba ikiwa ni pamoja na; laptop 24, simu
za mkononi 59, Televisheni 31 za aina mbalimbali, mitungi 31 ya gesi ya ujazo wa kg 16, kamera 9 na subwoofer 2, Baadhi ya vitu vilivyo kamatwa tayari vimetambuliwa wa wamiliki.


Jeshi la Polisi pia limewakamata na linawahoji kwa kina watuhumiwa watano kwa tuhuma za kupokea mali za kutoka kwa wezi hao na kuzifanya sehemu ya biashara zao.


Katika hatua nyingine, jitihada za kuzuia na kupambana na dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata muuzaji sugu wa bhangi Maneno Mayoge
Bundala mwenye miaka 28 mkazi wa Majimatitu, Mbagala, Temeke na wenzake wawili wakiwa na bhangi
gunia saba 07, puli 445, mbegu za bhangi kg 5 na magazeti ya kufungia bhangi wakiwa wamezificha kwenye nyumba yao.


Pia Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 03 waporaji wa mikoba kwa pikipiki vishandu.Pia imekamatwa Pikipiki namba MC. 252 DTG BOXER.


Kuelekea sikukuu ya Eid Alhaj, Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanasherekea kwa amani na usalama umeimarishwa kwa kiwango cha juu katika maeneo yote ya ibada, maeneo ya fukwe na mitaani. Waendesha vyombo vya moto wanaendelea kutahadharishwa
kufuata sheria na kujiepusha vileo wawapo na vyombo hivyo.


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawatakiwa wananchi wote sikukuu njema ya Eid Alhaj.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram