298 views 4 mins 0 comments

WAKUU WA WILAYA WAMEZIAGIZA TAASISI ZA TAMISEMI KUTEKELAZA MAJUKUMU YAO

In KITAIFA
June 27, 2023

Wakuu wa Wilaya za Lindi na Mtwara wameziagiza Taasisi zilizoko Mikoani humo kuhakikisha wanalipia gharama za huduma wanazopatiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ili kuuwezesha Wakala huo kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Wakuu hao wa Wilaya, wameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati wa vikao vya wadau vilivyoandaliwa na TEMESA na kufanyika katika Wilaya zao kwa lengo la kuendelea kupeana mrejesho baina ya TEMESA na wadau wake kwa ujumla ambao ni wauzaji wa vipuri, watengenezaji wa vilainishi, Taasisi za Umma na Serikali pamoja na watu binafsi ikiwa ni muendelezo wa jitihada za Wakala huo katika kuboresha utendaji kazi wake ili kuhakikisha wateja hao na Serikali wanawezeshwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi bila vikwazo vyovyote.


Akizungumza wakati wa Kikao cha wadau Mkoani Lindi, kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Tarehe 22 Juni, 2023, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga amewaomba wadau hao kuendelea kupata huduma TEMESA huku akiwataka kuhakikisha wanalipia gharama za huduma baada ya kumaliza kutengenezewa magari yao na mitambo


”Lakini tukipata huduma tulipe, Mheshimiwa Rais hawezi kuhudumia tu kila siku, hapana, itafika mahala Taasisi lazima ijiendeshe angalau kwa asilimia fulani, sasa hawawezi kuwa wanaenda kuchukua vipuri huko wakufungie halafu hulipi, wanakuja kukurekebishia wewe hulipi,wataishi vipi, na hawa tumewapa uwezo wa kufanya shughuli zao kutegemea na malipo ambayo wanayapata, kwahiyo tukalipe.”amesisitiza Ndemanga

na kuwataka TEMESA kuhakikisha wanakagua madeni hayo vizuri ili kuona namna yanavyoweza kulipika, amewaomba pia kutokataa kutengeneza magari ya Taasisi ambazo zinadaiwa.
Mkuu huyo wa Wilaya pia ameipongeza TEMESA kwa maboresho ambayo

Mkuu huyo wa Wilaya pia ameipongeza TEMESA kwa maboresho ambayo inaendelea kuyafanya katika karakana zake na kuziomba Taasisi za Umma na wadau kuiamini TEMESA kwakuwa imebadilika na inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

 ”TEMESA sasa imeboreka, kwa wale ambao tumepata nafasi ya kukagua na kusikiliza kule nje, sio TEMESA ile ambayo tulikuwa nayo miaka iliyopita, kwahiyo niwaombe tuondoe hofu, twendeni tupeleke magari yetu TEMESA, twendeni tuwaite maofisini kwetu warekebishe wakague viyoyozi, waje kwenye nyumba zetu waangalie pia umeme, wana vifaa vya kisasa vya kukagua na kutengeneza viyoyozi vyetu, wana vifaa vya kisasa vya kupima umeme kwenye nyumba zetu, twendeni tuwatumie TEMESA.” Amesema Ndemanga

na kuongeza kuwa Wakala huo kwa sasa umebadilika na gharama zake sasa zinaendana na soko tofauti na zamani huku akiwahakikishia wadau wa Mkoa wa Lindi ubora wa huduma kutoka Wakala huo.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Hanafi Msabaha, akizungumza na wadau hao  Mkoani humo mwishoni mwa wiki, amewataka wadau hao  kutokata tamaa na TEMESA, kurejesha imani yao kwa TEMESA na kuendelea kufanya kazi nao na kama itajitokeza changamoto basi wadau hao wasisite kuileta mbele yake ili izungumzwe na kutatuliwa.

Msabaha amesema vikao vya aina hiyo viwe endelevu kwa TEMESA kuendelea kukaa na wadau wake na kutathmini namna wadau hao wanavozitafsiri huduma za Wakala, wapi wanakosea na wapi wapaboreshe zaidi ili TEMESA iendelee kutoa huduma bora. Msabaha pia amesisitiza suala la wadau hao hasa Taasisi za Umma kulipa madeni yao kwa wakati.


”Lakini ndugu wadau, tunapopata huduma za TEMESA basi mimi niwaombe na sisi tuwe waaminifu tulipe mapema, na mara nyingi Taasisi za Serikali na Wakala za Serikali zinazotoa huduma zinakwama kwasababu hiyo, Taasisi ni za kwetu wenyewe lakini tunakopa hatulipi, lakini mjue kwamba kuwa na madeni mengi pia inasababisha Taasisi kushindwa kujiendesha.” Alimaliza Msabaha.

/ Published posts: 1926

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram