229 views 3 mins 0 comments

UNDP:kuibua sauti kutoka kwenye nyanja mbalimbali na kupeana uzoefu,

In KITAIFA
June 26, 2023

Naibu katibu mkuu wa wizara ya viwanda na biashara Dr.Hashili Abdallah amesema Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan,kwa jitihada zake za kuifungua nchi ambapo tumeshuhudia ujio wa wawekezaji mbalimbali kutoka nje ya nchi wakija kuwekeza hapa nchini. Miongoni mwa jitihada za makusudi zilizotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita ni pamoja na kufanya mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali zinazosimamia sekta ya uwekezaji na biashara nchini. Jitihada hizo za Serikali zimechangia kukuza uwekezaji hususan katika Sekta ya Viwanda ambako kumechangia kupanua wigo wa kodi za Serikali na kuongeza wigo wa ajira kwa watanzania.

Akizungumza Jijini Dar es salaam Naibu katibu mkuu wa wizara ya viwanda na biashara Dr.Hashili Abdallah amesema katika mkutano wa wadau wa kupata maoni kuhusu Taarifa ya Tathmini ya Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji na Miradi ya Kimkakati (Assessment of Local Content in Tanzania).

“Dhana ya ushiriki wa watanzania inalenga katika kuhakikisha kuwa, thamani ya ziada inayotokana na miradi ya kimkakati na uwekezaji inabaki nchini na kuchangia katika ukuaji wa uchumi”.

“Utekelezaji wa dhana hii ni jitihada za makusudi zinazofanywa na Serikali ili kuhakikisha ajira kwa watanzania; uanzishwaji wa kampuni za ubia; matumizi ya malighafi za ndani katika uzalishaji na utoaji wa huduma; masoko ya uhakika ya bidhaa na huduma zinazozalishwa au zinazotolewa na kampuni za kitanzania; uhawilishaji wa teknolojia; ushiriki wa kampuni za kitanzania; na ushirikishwaji wa jamii zinazoishi katika maeneo ya uwekezaji au miradi inapotekelezwa na kunufaika kiuchumi”.Alisema Abdallah

Hata hivyo Abdallah amesema Dhana ya ushiriki wa watanzania katika uwekezaji na miradi ya kimkakati Tanzania ilianza kujadiliwa kwa kina mwanzoni mwa miaka ya 2000. Hali hii ilitokana na kutokuwepo kwa Sera au Sheria zilizokuwa zimebainisha ushiriki wa watanzania katika sekta mbalimbali za kiuchumi kutokana na kugundulika kwa rasilimali nyingi hasa mafuta, gesi na madini nchini.

Serikali imechukua hatua za makusudi zinazolenga kukuza ushiriki wa watanzania na kuhakikisha kuwa miradi ya kimkakati na uwekezaji unanufaisha watanzania kupitia ajira; uanzishwaji wa kampuni za ubia; matumizi ya malighafi za ndani katika uzalishaji na utoaji wa huduma; masoko ya uhakika ya bidhaa na huduma zinazozalishwa au zinazotolewa na kampuni za kitanzania; na uhawilishaji wa teknolojia. Aidha, mapato yatokanayo na shughuli za uwekezaji na miradi ya kimkakati yanufaishe watanzania na Taifa kwa kupata maji safi na salama, huduma bora za afya, elimu bora na miundombinu madhubuti.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram