192 views 3 mins 0 comments

MSIGWA:Mkataba huu ni wa ushirikiano serikali na serikali

In KITAIFA, Uncategorized
June 24, 2023

Msemaji mkuu wa serikali Leo tarehe 24 jumamosi juni 2023 ameongea na waandishi wa habari Katika ofisi za idara ya habari maelezo zilizopo posta Jijini Dar es salaam Akizungumzia juu ya maswala ya uwekezaji bandarini.

Msigwa amesema Hali ya nchi yetu Kwa ujumla ipo shwari serikali inazidi kutoa huduma za kijamii kama kawaida ambazo ni Huduma za utawala,Utekelezaji WA maendeleo na kutatua kero mbalimbali

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa ameendelea kuwatoa hofu Watanzania kuhusu sakata la uwekezaji katika Bandari akieleza kilichosainiwa ni makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai na si vinginevyo.

Amesema ushirikiano huo unalenga kupata manufaa ya kiuchumi na kijamii katika uendeshaji, uboreshaji na uendelezaji wa bandari nchini Tanzania na siyo kweli kwamba bandari imeuzwa.

“kumekuwa na mijadala mkubwa kupitia vyombo vya habari kuhusiana na bandari ni kweli serikali kupeleka mkataba WA makubaliano Bungeni Kwa ajili ya kulidhiwa ikiwa ni wajibu WA katiba Katika idala ya 63 na idala ndogo ya 3 inaelekeza kwamba ukitaka kukubaliana kati ya serikali na serikali basi makubaliano hayo yanaitaji kupata maridhiano na kupata baraka za bunge”. amesema msigwa

Kauli hiyo ameitoa wakati kukiwa na mjadala kutokana na Serikali ya Tanzania kuwa na nia ya kuruhusu uwekezaji katika Bandari, huku kampuni ya DP World kutoka Dubai ikitarajiwa kupewa dhamana hiyo.


Msigwa amesema baada ya makubaliano hayo ya ushirikiano ndipo itakuja mikataba ya utekelezaji wa namna ya uendelezaji wa bandari nyaraka hizo zitakwenda Katika mkataba ya nchi mwenyeji ambayo inayoitwa(HostGoverment Ingredient)

โ€œWataalamu wetu chini ya Wizara ya Uchukuzi wataingia kwenye majadiliano ya kina ya miradi mahsusani. Watanzania msiwe na hofu yoyote, Serikali yetu chini ya Rais Samia Suluhu Hassan iliona mapema tangu alipoingia mwaka juzi kwamba bandari zetu hazina ufanisi, hivyo tuna kazi ya kuziboresha ili zitupe ufanisi kwa kutengeneza mapato ya kutosha”.

โ€œBandari ya Dar es Salaam pamoja na kuwa na fursa kubwa ya kuhudumia nchi nane lakini mapato tunayopata ni kidogo. Mapato ya forodha tunapata Sh7.7 trilioni wakati wataalamu wanasema tukiwekeza tunaweza kupata Sh26.7 trilioni,โ€ amesema”amesema msigwa

Amesema lengo la Serikali ni kuongeza uwezo wa bandari ili nchi itoke kwenye kuhudumia mizigo tani 18 milioni kwa mwaka hadi kufikia tani 50 milioni na zaidi.

“Jiji la dar es salaam kama munavyolijua ndio Jiji letu kubwa la kibiashara ambalo ndio kitovu kikubwa Cha uchumi Katika nchi yetu shughuli za mikoa wa dar es salaam zinaendelea kama kawaida chini ya mkuu wa MKOA Albert chalamila”amesema msigwa

Madina Mohammed

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram