286 views 47 secs 0 comments

NI MAKOSA KUJIHUSISHA NA BIASHARA NDOGO ZA HUDUMA ZA FEDHA BILA LESENI YA BENKI KUU

In KITAIFA, Uncategorized
June 22, 2023

Benki Kuu ya Tanzania imebaini kuwa kuna baadhi ya taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila ya kuwa na leseni, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.

Taarifa hiyo imetolewa na Gavana WA Bank kuu ya Tanzania anawasamba taasisi, kampuni na mtu binafsi wasio na
leseni hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha. Kufuatia kifungu cha 16(2)(a) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018,

Amesema hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa Sheria hiyo ni pamoja na faini isiyopungua Shilingi Milioni 20 au kifungo cha muda usiopungua miaka miwili.


Benki Kuu ya Tanzania inawakumbusha watoa huduma ndogo za fedha waliokwisha kupata leseni
kufuata sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania ikiwemo kuwapa wakopaji mikataba, kuonyesha riba ya mkopo kama ilivyopitishwa kwenye sera ya mkopo, gharama nyingine zote wanazotoza, na riba kukokotolewa kwa mwezi na sio kwa siku.


Aidha Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuwaasa wananchi kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi,kampuni au mtu binafsi ambao hawana leseni.

Pia ameongeza Kwa kusema orodha ya taasisi, kampuni na watu binafsi wenye
leseni za biashara ya kukopesha zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania inapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu ambayo ni www.bot.go.tz na kwenye matawi yake yote.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1212

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram