Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward mpogolo amefanya mahojiano na waandishi wa habari Katika ofisi zake Leo tarehe 22,2023 zilizopo Jijini Dar es salaam Akizungumzia mambo mbalimbali yakihusiana na mambo yake ya kazi na Moja ya mambo hayo na uwekezaji wa bandari akitoa ufafanuzi
Wakati shughuli ya sakata la bandari likiwa linaendelea kila Kona watu wakiwa wanalizungumzia wanasiasa nao wanalizungumzia Katika nyanja zao na pia wakitoa malalamiko Yao kuhusiana na sakata la uwekezaji bandarini limeweka sura mpya Kwa kila mtanzania na mkuu wa wilaya ya Ilala Edward mpogolo ameyasema hayo.
“Kwa mwanadamu ambaye ameshindwa kuwa mstaarabu wakati anatoa maoni yake huyo anapaswa kusamehewa kwani maandiko ya dini yanasema msamehe mtu mara 70,ukigungua mwezio amekukosea”.Alisema mpogolo
mpogolo amesema hao wanasiasa wanaoongea hivyo hawana lengo kwani Rais Samia Suluhu Hassan yeye analengo na lengo lake lipo Katika ilani ya uchaguzi,Mhe.Rais Samia aliwaahidi watanzania Katika miradi ambayo anayoishughulikia na serikali ikiwemo eneo la bandari,mradi wa Reli na upatikanaji wa umeme na kwenye Ajira na miradi mingine ambayo Bado inatekelezwa.
“Mkataba ambao Rais Samia Suluhu Hassan ameuweka Kwa wananchi kwa miaka mitano unalenga miundombinu ya nchi Sasa hao wanasiasa ambao wanaopinga hawana malengo wanachokitaka ni kumfanya Rais Samia Suluhu Hassan asifikie Katika malengo kwasababu wanajua akifika Katika malengo watanzania watampa mitano tena na kumfanya ni kumzuia Katika malengo ambayo anataka kuyafikia”. Alisema mpogolo
Aidha mpogolo amesema kutoa maoni ni haki ya kila mtanzania ndomana Rais Samia ametaka Kwa kila mtanzania kutoa maoni na maoni yenyewe utoe ya yenye staha na usitoe maoni ambayo unaona yanaonesha kugawa Tanzania,Udini,Makabila na Jinsia kwani huwezi kutoa maoni ambayo yanakizana na mambo hayo na Mhe.Samia Anasimamia lengo lake ambalo amepewa na chama Cha mapinduzi na lengo ambalo amepewa na wananchi wa Tanzania
“Tukijiuliza tulipoenda mwaka 2020 wale wote ambao munaowaona wanasiasa nao walipeleka malengo Yao kama haya Kwa watanzania na walipopeleka hawajakubalika na lililokubalika hili lengo la Mhe.Rais Samia ndilo ambalo tunaloliishi na tumuache afanye na tumsapoti Kwa sababu Nia yake na dhamira yake ni njema”. Amesisitiza mpogolo
Hata hivyo mpogolo amesema Rais Samia hawezi kuacha Tanzania inaharibika tumeona pale bandarini wametolewa wakurugenzi wakuu wangapi Rais Samia ameliona tatizo lipo wapi na kitu ambacho tunachokipata ni malalamiko na kuona Moja wapo ni uwezo WA bandari yetu kuhudumia wateja wetu ambao wanaokuja na maswala ya miundombinu na teknolojia ndo mana Mhe.Rais akaamua kumtafuta mwekezaji na kuingia nae ubia Ili kupata Fursat ya kuendeleza bandari yetu.
Na miradi yote mikubwa Mhe.Rais yote yupo Katika hatua za mwisho kutimiza na miradi hiyo yote IPO kwenye ilani.
Mpogolo ameongeza kuwa hakuna mtu atakae penda bandari ya Dar es salaam Iboreshwe na ikiboreshwa bandari za pembezoni watu hawatafaidika sana lakini kwenye historia Tanzania tunamahusiano mazuri na nchi mbalimbali duniani ikiboreshwa bandari ya Dar es salaam kulivyokuwa na amani na bandari ya Tanga na ya Mtwara na watu wengine watakimbia Katika nchi zao na kuja Katika nchi yetu ya Tanzania na ndomana Kuna vita ya kiuchumi na ya kisiasa
Pia ametoa wito Kwa watanzania kuwa sisi tuendelee kumsapoti Mhe.Rais na serikali yake kuhakikisha kuwa bandari inaboreshwa Kwa ubia kwasababu Mhe.Rais Samia anayo malengo ya kuitumikia watanzania hao wanaopinga hawana malengo.
Madina Mohammed