99 views 2 mins 0 comments

Serikali wasiwe kikwazo kutoa ushirikiano kwa viongozi WA dini

In KITAIFA
June 20, 2023

WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano WA Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa amewataka watendaji wa Serikali wasiwe kikwazo na waendelee kutoa ushirikiano viongozi wa dini na wawekezaji wa ndani na nje ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 40 ya International Evangelism Centre kilichoko Sakila jijini Arusha
Amesema Serikali itaendelea kujenga mazingira bora ya uwekezaji na kushirikiana na sekta binafsi pamoja na madhehebu yote ya dini katika kutekeleza majukumu mbalimbali.

“Katika hili nasisitiza watendaji wote wa Serikali kuendelea kuziunga mkono taasisi binafsi zinazotoa huduma kwa wananchi ili ziweze kutimiza malengo yake.”alisema waziri Majaliwa

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza Askofu Mkuu wa Makanisa ya International Evangelism na Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Eliud Issangya kwa kuongoza vema chuo hiko ambacho kimetimiza miaka 40.

“Nimefurahi sana kusikia idadi ya wahitimu wa chuo hiki imefikia zaidi ya 10,000 ama kwa hakika mmeweza kuweka hazina kubwa ya watendaji katika shamba la Mungu.”aliongezea waziri Majaliwa

Aidha mkuu wa Chuo hicho askofu issangya Akizungumzia changamoto mbalimbali zinakikabili chuo hicho ikiwemo ya barabara, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa TARURA mkoani Arusha kuhakikisha barabara hiyo ya kutoka Kikatiti hadi Sakila kukarabatiwa.

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la International Evangelism la nchini Congo, Askofu Byamungu Magala ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu.

“Tanzania ni Taifa ambalo limejaa amani na utulivu na ni Taifa ambalo halina ubaguzi wa dini wala kabila, Taifa zuri linalopokea wageni bila ya shida yoyote. Nawapongeza viongozi wa Taifa hili.”

“Kila ninapokuja hapa namuomba Mungu nasi atupe amani. Amani hii mliyonayo mnatakiwa kuilinda kwa sababu Taifa bila amani raia watakuwa na matatizo makubwa, sisi watu wanauawa kinyama.”alisema magala

Pia, amempongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi mahiri na kumtuma Mheshimiwa Waziri Mkuu kuhudhuria sherehe hizo. “Hali hii inaonesha namna ambavyo viongozi wa Serikali wako karibu na raia na wanyenyekevu sana tofauti na kwetu.”

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram