188 views 3 mins 0 comments

Rc chalamila ATOA onyo Kali watakaojihusisha na upigaji

In KITAIFA
June 20, 2023

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameonya vikali watumishi na madiwani watakao jihusisha na ‘upigaji’ fedha katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, huku watumishi watatu wa jiji hilo wakisimamishwa.


Amewataka Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Jomaary Satura, kuwachukulia hatua kali watendaji wasio wajibika na wasipo fanya hivyo atawachulia hatua viongozi hao.


Alitoa onyo hilo alipokuwa akizungumza katika Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo ambacho kilijikita kujadili hoja za Msimamizi na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Chalamila alisema, katika ripoti hiyo ya CAG eneo la ukusanyaji wa mapato limebainishwa kuwa na changamoto nyingi zikiwemo hoja 13.


“Tunatakiwa kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha hoja hizi hazijirudii tena. Mkurugenzi weka nguvu kubwa kushughulikia ukaguzi. Vikwazo hivyo vihudhuriwe nawe na wakuu wa idara pasipo kukosa.”alisema Chalamila.


Akizungumzia ukusanyaji mapato, Chalamila alisema kunachangamoto katika eneo la mapato ya huduma za jamii.
“Mfano katika eneo hili Halmashauri ilikusanya sh. biloni 1.2. Katika fedha hio sh. bilioni 1 zilitolewa na Bandari ya Dar es Salaam n ash. milioni 200 tu ndiyo zilizokusanywa katika huduma nyingine,”alibainisha.
Chalamila alibainisha baadhi ya maofisa wa mapato katika halmashauri wanambinu zisizo faa.


“Mtu anayetakiwa kulipa sh. milioni 300 anaweza kuwalipeni nyie sh. milioni 100 na deni likafutika kienyeji. Haya ni maeneo ambayo lazima tuumizane.Na nimemwambia mkurugenzi usipochukua hatua wewe mimi nitakuchukuli hatua wewe. Nimemwambia Mkuu wa Wilaya usipochukua hatua wewe mimi nitakuchukulia hatua wewe,”alibainisha chalamila


Amtaka mkurugenzi kudhibiti upotevu wa fedha za umma.
Alitolea mfano wa ukusanyaji wa fedha za malori y a migo yanyoingia katikati ya jiji.


“Usiku makontena yanakusanya fedha nyingi lakini hazingii katika akaunti ya halmashauri. Na huo mnyororo wote naufahamu. Nafahamu hata fedha ya maegesho inayokusanywa na Tambaza (Kampuni ya udalali) zinakoelekea,”alisema Chalamila.


Aliongeza; “Ninacho kitafuta hapa ni ili nipige pingu vizuri. Nafahamu mnyororo mpaka walioondoka na waliopo. . Fedha inakusanywa saa ngapi na jinsi inavyo chukuliwa,”
Alionya madiwani kuto kushiriki katika ubadhirifu huo badala yake kusaidia kuleta mabadiliko.


Nae Mkurugenzi wa jiji hilo Satura alisema tayari hatua zimeanza kuchukulia ambapo wafanyakazi watatu, akiwemo aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ukusanyaji mapato ya huduma na eneo la makontena.


“Kikao cha menejimenti kilibaini kuwepo kwa mapungufu na tutaendelea kufanya hivyo,”alisema Stura.


Aidha Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, alisema jiji hilo litaendelea kusimamia kasi ya maendeo kwa kushirikiana na Jiji la Busati la Korea Kusini baada ya kuingia nalo makubaliano.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram