Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewatuliza wapangaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la kariakoo na kuwataka kufuata sheria na mikataba waliyoingia na shirika hilo.
Akizungumza jijini dar es salaam na wapangaji hao leo tarehe 19 Juni 2023 kwa kusikiliza kilio cha wapangaji hao Waziri WA ardhi nyumba na maendeleo ya makazi dkt mabula Amesema waliotaka kuongezewa muda wa notisi ya miezi mitatu waliyopewa na NHC kupisha uwekezaji.
Kwa mujibu wa wapangaji hao wa eneo la Kariakoo, hawapingani na uwekezaji unaofanywa na serikali bali wanachotaka ni kushirikishwa, kuongezewa muda wa notisi sambamba kupewa kipaumbele cha kupangishwa pale mradi utakapokamilika.
Akijibu maombi ya wapangaji hao, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewaambia wapangaji hao kuwa, katika suala la uendelezaji milki, Kariakoo ni eneo litakalofanyiwa maboresho makubwa na halitarudi katika hali yake ya sasa bali itakuwa na maboresho ya majengo.
“hakuna mkataba uliosainiwa na wala muundo wa majengo uliowekwa na Shirika la Nyumba la Taifa ambapo ameweka wazi kuwa wanaodai kupewa ubia na kuanza kukusanya fedha ni matapeli wanaotakiwa kuchukuliwa hatua”.
‘’Kwanza nashangaa mtu kujitambia na kuanza kukusanya fedha hata kabla ya kuwa na uhakika unayekusanya pesa zake atakuwa mpangaji’’. Alisema Dkt Mabula
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mkataba ulioingiwa baina ya Shirika la Nyumba la Taifa na Wapangaji una kila kitu na mpangaji anatakiwa kukijua ambapo aliwataka wanasheria wanaowashauri wateja wao kuhakikisha wanawashauri kwa kuzingatia mikataba badala ya kuwapa matumaini na kuleta taharuki.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah alisema, anachofurahishwa ni kwamba serikali na wapangaji wa eneo la kariakoo wanakubaliana na uendelezaji unaotaka kufanyika na tofauti ni namna ya eneo hilo linavyoendelezwa.
‘’Kwa kweli hapa nashukuru sana serikali na wapangaji wa eneo la kariakoo tuna dhana moja ya kukubali kariakoo kuendelezwa’’. Alisema Abdallah
Madina Mohammed