104 views 4 mins 0 comments

Wanawake watakiwa kuwa makini na raia WA kigeni

In KITAIFA
June 19, 2023

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama imefanya operesheni katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro na Arusha na kufanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya heroin kilogramu 200.5, bangi kavu iliyokuwa tayari kusafirishwa gunia 978, bangi mbichi gunia 5,465, bangi iliyosindikwa (skanka) kilogramu 1.5, methamphetamine gramu 531.43, heroin kete 3,878, cocaine kete 138, mililita 3,840 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Pethidine pamoja na kuteketeza ekari 1,093 za mashamba ya bangi.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini dar es salaam kamishna jenerali WA mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) Aretas lyimo Amesema Kwa kushirikiana na Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (INCB) Mamlaka imezuia kuingia nchini jumla ya kilogramu 1,507.46 za kemikali bashirifu ambazo zingeweza kutumika kutengenezea dawa za kulevya.

“Ukamataji huo umefanyika kuanzia tarehe 25 Machi, 2023 hadi tarehe 19 Juni, 2023 unawahusisha watuhumiwa 109 wakiwemo raia watatu wa kigeni na
Baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa mahakamani na wengine wanatarajiwa kufikishwa mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika”.

“Kutokana na udhibiti kuwa mkubwa, wafanyabiashara wa dawa za kulevya wameendelea kubuni mbinu mpya za usafirishaji wa dawa za kulevya ili kukwepa kukamatwa”. Amesema Lyimo

Mamlaka imebaini mbinu hizo na kuchukua hatua. Mbinu mojawapo inayotumika ni raia wa kigeni kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na wanawake wa kitanzania zaidi ya mmoja na kuficha dawa za kulevya kwenye makazi ya wanawake hao huku wao wakipanga nyumba tofauti na wanakoishi wapenzi wao.

Pia amewaomba Wanawake wanatakiwa kuwa makini zaidi kwani katika baadhi ya matukio, wamekuwa wakitumiwa na wapenzi wao hasa raia wa kigeni kusafirisha na kupokea mizigo wasiyoijua na wakati mwingine mizigo hiyo huwa na dawa za kulevya na hivyo hujikuta matatani.

“Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kinaeleza kwamba, ni kosa kusafirisha dawa za kulevya, na mtu yoyote akithibitika kutenda kosa hilo atawajibishwa kisheria ikiwa ni pamoja na kifungo kisichopungua miaka 30 au kifungo cha maisha gerezani”.amesisitiza lyimo

Aidha ameongeza kuwa Serikali imejipanga ipasavyo kuhakikisha inamaliza tatizo la dawa za kulevya kwa ustawi wa jamii. Kutokana na kuwepo madhara makubwa ya kiuchumi, kijamii na kisaikolojia yanayotokana na matumizi ya dawa za kulevya, ni vema wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kuwafichua wote wanaojihusisha na matumizi na biashara ya dawa za kulevya ili kwa pamoja tuweze kulikomboa taifa kutoka katika janga hili.

Lyimo Ameongeza kuwa Ili kupanua wigo wa utoaji elimu, Mamlaka imeingia makubaliano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutumia klabu zao zilizokwisha anzishwa kwenye shule na vyuo Kwa kutoa elimu ya juu ya tatizo la dawa za kulevya.

Maadhimisho haya kwa mwaka huu kitaifa, yatafanyika tarehe 23 Juni, hadi tarehe 25 Juni, 2023 jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Maadhimisho haya yataambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali za udhibiti zinazofanywa na Mamlaka pamoja na wadau wake katika udhibiti wa dawa za kulevya na utoaji elimu kuhusu tatizo la dawa za kulevya.

Mgeni rasmi siku ya kilele tarehe 25 Juni, 2023 ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni โ€œTuzingatie Utu na Kuboresha Huduma za Kinga na Tiba

Na Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram