252 views 31 secs 0 comments

SERIKALI KUWATHAMINI WATU WENYE ULEMAVU

In KITAIFA
June 19, 2023

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwajali na kuwathamini Watu wenye Ulemavu kwa kuhakikisha inakuza ustawi wa kundi hilo.


Akizungumza Katika viwanja vya Bungeni jijini dodoma Naibu waziri Mhe.patrobas Katambi alipokutana na wageni kutoka Chama cha Wazazi wa Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBAHT) amesema kuwa Serikali imeboresha huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ambapo mwaka 2022/2023 ilitenga jumla ya shilingi bilioni 3.46 kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa vyuo vya Watu Wenye Ulemavu vya Mtapika (Masasi – Mtwara), Luanzari (Tabora), Sabasaba (Singida) na Yombo (Dar es Salaam).

“Serikali katika mwaka 2023/2024 imepanga kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kujiajiri na kuajiriwa kwa kuongeza fursa za mafunzo ya ufundi stadi na marekebisho”Alisema katambi

Kwa upande mwengine Mhe. Katambi amesema Serikali imetengeneza Mfumo wa Kielektroniki wa Watu Wenye Ulemavu ili kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa taarifa za watu wenye ulemavu. Mfumo huo utawezesha kumtambua mtu mmoja mmoja mwenye ulemavu, mahali alipo,na shughuli anayoifanya na mahitaji yake

Madina Mohammed

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram