Azam media Kwa kushirikiana na studio za powerbrush kuzindua onyesho la kwanza la kihistoria ambalo litakalofanyika siku ya ijumaa Juni 23,2023 ambalo litakalo fanyika Katika ukumbi WA century sinemax mlimani city dar es salaam.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini dar es salaam Afisa muendeshaji mkuu Azam yahya Mohammed Amesema tutumie fursa hii Kwa niaba ya Azam media na powerbrush studio kutambua mchango mkubwa WA serikali yetu Katika kusimamia Michezo na Sanaa Nchini na kuweka mipango endelevu ambayo tunashuhudia matunda yake kupitia mageuzi haya kwenye tasnia ya filamu nchini
“Bodi ya filamu wamekuwa mhimili mkubwa Katika kutoa hamasa,kuratibu njia sahihi za kuisukuma Sanaa yetu ya filamu na kipekee kabisa tunasema Asante Sana Rais WA Jamhuri ya Muungano WA Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kuweka chachu inayopelekea Sasa Sanaa yetu ya filamu kimataifa”. Amesema Mohammed
Aidha Mohammed Amesema lengo letu ni kuhakikisha maonyesho haya ya Katika majiji yetu yanaleta ulimwengu WA kuvutia WA filamu za kisayansi na kuibua ubunifu na shauku ya kutazama filamu zote kupitia filamu yetu ya EONII.
Naye katibu mtendaji WA bodi ya filamu Dr.kiagho kilonzo Amesema bodi ya filamu ilibuni programu maalum ya kurekebisha Utamaduni WA kuangalia filamu kwenye kumbi za sinema yenye lengo la kuongeza Pato Kwa waandaaji WA filamu hapa nchini pamoja na wacheza filamu.
“ni filamu iliyobeba maudhui ya ugunduzi WA kisayansi Katikati ya uhitaji WA nishati ya uhakika na ombi kubwa la kukosekana kwake kunakozua taharuki Katika jamii husika”.
“Filamu hii inalenga kuonyesha vipaji na uwezo mkubwa ndani ya tasnia ya filamu Tanzania Kwa kuonyesha madoido na ujongevu (animations) za kisasa zinazotumika kuzungumzia mkasa huu”.Alisema kilonzo
Hata hivyo kilonzo ameongeza kuwa duniani kote pamoja na uwepo WA hiyo mifumo ya kidijitali Bado uonyeshaji WA filamu kwenye kumbi za sinema kunapewa nafasi kubwa ndio maana serikali inaungana na kampuni ya azam media kuonyesha filamu Yao hii iitwayo EONII kwenye kumbi za sinema zilizoko hapa nchini.
Filamu ya EONII imegharimu takribani Dola laki mbili (USD 200.000) za kimarekani na imetengenezwa Kwa kipindi Cha miaka minne