298 views 15 secs 0 comments

SERIKALI NA CCM KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO NCHINI

In MICHEZO
June 17, 2023

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu amekutana na wajumbe kwa kufanya kikao cha pamoja na ujumbe kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo wamejadili namna bora ya kuboresha miundombinu ya michezo nchini.

Akizungumza jijini Dodoma ambapo timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wake Bw. Saidi Yakubu na ujumbe wa CCM ukiongozwa na Bw. Mussa Matoroka MNEC na Katibu wa CCM mkoa wa Arusha.


Amesema Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili kuhusu uendeshaji na usimamizi wa viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na kusimamiwa na Serikali pamoja na CCM ambavyo vinatumika katika michezo mbalimbali nchini ikiwemo Ligi Kuu ya NBC.

Hata hivyo Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe nane kutoka CCM akiwemo Mhasibu Mkuu wa CCM Taifa Bw. Thobias Abwalo huku ujumbe wa Wizara yenye dhamana na michezo ikiwa na wajumbe saba akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Ally Mayayi.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram