268 views 48 secs 0 comments

RC MTANDA AGEUKA MBOGO UHARIBIFU WA MAGARI, AFANYA OPARESHENI YAKUSHTUKIZA SERENGETI.

In KITAIFA
June 17, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mtanda ameendesha operesheni ya ukaguzi wa magari ambayo hayafanyi kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kutoa maagizo kwa Afisa Usafirishaji na Wakuu wa Idara husika kuhakikisha magari hayo yanatengenezwa haraka na kwa kipindi walichokubaliana.

Rc Mtanda amesema kumekua na tabia ya kutelekeza magari ya serikali ili kwa hapo baadae wajiuzie kwa gharama rahisi.

“Sasa kwa Mkoa huu wa Mara nitayasimamia magari yote yaliyotelekezwa yatengenezwe na yataendelea kufanya kazi.” Amesema Mhe. Mtanda ameendesha zoezi hilo la kustukiza mara baada ya kumaliza kikao kifupi cha watumishi wa Wilaya ya Serengeti.

Editor / Published posts: 21

Journalist

Twitter
Facebook
Youtube
Linkedin
Instagram