146 views 3 mins 0 comments

Karibu wa kamati maalum ya NEC awasihi wananchi wa Zanzibar kuepuka upotoshaji

In KITAIFA
June 17, 2023

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar Khamis Mbeto Khamis,amewasihi wasomi nchini kufanya utafiti wa kina wa kufuatilia na kutathimini kitaalamu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ili wananchi wajue mafanikio hayo.

Akizungumza katika kongamano la kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi, la kuelekea miaka mitatu ya uongozi wake lililoandaliwa na Tawi la Seneti ya UVCCM Mkoa wa Kusini Unguja Skuli ya Biashara ya SOB SUZA iliyopo Chwaka.

Khamis mbeto Alieleza kuwa utafti huo utawasaidia wananchi kuepuka upotoshaji unaofanywa kwa sasa na baadhi ya viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo kupitia mikutano yao ya hadhara iliyofanyika kisiwani Pemba.

Mbeto, alisema Zanzibar imepiga hatua kubwa za kimaendeleo chini ya uongozi wa Dk.Mwinyi,hivyo wanasiasa na viongozi wa upinzani wanatakiwa kuthamini na kuunga mkono juhudi hizo badala ya kubeza na kupuuza juhudi hizo kwani nao ni miongoni mwa wanufaika wa maendeleo hayo.

“Wasomi msikubali kudanganywa fanyeni utafiti juu ya kazi kubwa iliyofanywa na Dk.Mwinyi toka aingie madarakani mpaka Sasa, leteni majibu na kuibua hoja makini za kujenga mshikamano na maridhiano ya kisiasa yanayohimiza ukuaji wa uchumi wa nchi”.

“Wapinzani tunajua hawawezi kumpongeza wala kusifu juhudi hizo lakini japo mtathamini na kuheshimu mamlaka za kiutawala,kwani nanyi ni wanufaika juu ya maendeleo hayo kwani ruzuku,mishahara na huduma zote muhimu za kibinadamu zinazofanywa na Serikali nanyi mnapata kama wananchi wengine”,alisema Mbeto.

Pamoja na hayo Dk.Mwinyi, aliwasihi vijana hao wa idara ya UVCCM wa Vyuo Vikuu nchini kusoma kwa bidii ili wawe wazalendo wa kweli na waelekeze nguvu zao kusomea fani zinazoendana na mahitaji ya soko la ajira nchini zikiwemo za masuala ya Uchumi wa buluu zilizobeba utalii,mafuta na gesi.

Aidha Mbeto alieleza kwamba Serikali ya awamu ya nane chini ya Uongozi wa Dk.Hussein Ali Mwinyi, inatekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 katika sekta mbalimbali nchini.

Hata hivyo mbeto alisema kuelekea miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dk.Mwinyi, tayari amejenga skuli za kisasa kuanzia ngazi za msingi hadi Vyuo Vikuu ili vijana wasome katika mazingira rafiki yanayoendana na mahitaji ya kitaaluma.

Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC Mbeto, aliwasihi wananchi wasikubali kupotoshwa kwani nchi ipo salama na inapiga hatua kubwa katika nyanja za kiuchumi,kijamii,kisiasa,kiutamaduni na michezo.

/ Published posts: 1435

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram