305 views 2 mins 0 comments

Jeshi la polisi latoa onyo Kali la maandamano siku ya Jumatatu

In KITAIFA
June 17, 2023

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawatahadharisha wananchi kuhusu taarifa zinazozagaa kutoka kwa mtu mmoja kuwa kutakuwa na maandamano siku ya Jumatatu ya tarehe 19 mwezi huu ya kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi WA habari jijini dar es salaam kamishna msaidizi muandamizi WA jeshi la polisi Murilo Jumanne Murilo amesema kuwa Taarifa hiyo anayodai aliifikisha Polisi, tayari ameshajibiwa kwa kuyapiga marufuku maandamano aliyokuwa anataka kuyaratibu na kushauriwa kama ana jambo la msingi atumie vyombo mbalimbali vya kisheria anavyoweza kufika na kuwasilisha hoja zake bila maandamano ili haki zingine za wananchi za kufanya kazi wakiwa huru zisiingiliwe.

“Jeshi la Polisi linawatahadharisha watu kutoshiriki hicho kinachodaiwa maandamano na badala yake mnahimizwa kuendelea na shughuli zenu za kiuchumi na kijamii bila hofu. Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kwa mtu au kundi la watu linalotaka kuzusha taharuki kwa kuzuia watu wengine kufanya kazi zao”.Alisema Murilo

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 10 wanaodaiwa kuhujumu kwa kuiba miundombinu ya vifaa mbalimbali vya minara ya mawasiliano ya simu. Watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia opeshereni maalum kali iliyoanza tarehe Juni 5, 2023 na inaendelea katika jiji la Dar es Salaaam na mikoa jirani

Aidha watuhumiwa hao Waliokamatwa ni pamoja na Husein Ally Kijingo mwenye miaka (32) Mkazi wa Mbande Kisewe akiwa na wenzake 7 ambao wamekuwa wakiiba betri muhimu na vifaa mbalimbali vya minara ya mawasiliano ya simu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani.

Aidha Jeshi la polisi limewakamata pia Simon Mangu mwenye miaka (33) mkazi wa Ubungo na mwenzake mmoja baada ya kukutwa na vifaa vya minara ya mawasiliano ya simu vya wizi vinavyoibwa na kufichwa katika maeneo ya Mbezi Luis.

Katika hatua nyingine Jeshi la polisi katika Operesheni yake wamekamata jumla ya betri 68 zenye thamani ya Tsh 163,200,000 na vifaa mbambali vya minara ya mawasiliano ya simu vilivyoibwa na magari mawili yanayotumiwa na wezi hao kubebea vifaa hivyo ambalo ni Toyota Hilux T.850 BDR, Toyota Carina T.112 BRN na pikipiki MC.901 DJQ, na vifaa mbalimbali vya kuvunjia sehemu ya tukio.

/ Published posts: 1886

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram