479 views 2 mins 0 comments

YANGA SIYO MABINGWA MARA 29/ ACHENI KUPOTOSHA

In MICHEZO
June 15, 2023


Vita ya soka haijawahi kuisha nchini kuanzia ndani uwanja mpaka mtaani kwa mashabiki. Maafisa Habari nao hawajawahi kupoa, ‘Ukiufumba na Kufumbua’ unakutana na taarifa kedekede zilizojawa kejeli, majigambo, utani kiasi kuhusu vilabu vyao vyenye mamilioni ya mashabiki nchini.

Thabith Zakaria maarufu kama Zaka za Kazi ambaye ni Mkuu wa Idara ya Habari na mawasiliano Azam Fc ametoa hoja iliyochochea mijadala mizito kwenye vijiwe mbalimbali vya mashabiki wa soka nchini hasa mashabiki wa vilabu vya Mpira wa miguu cha Simba na Yanga, wengine wakiamini ni njama za afisa huyo kuwafanya wawe wanyonge.

“YANGA SIYO MABINGWA MARA 29 NA SIMBA SIYO MABINGWA MARA 22” Thabith Zakaria
Nitaarifa iliyoandikwa kwenye ukurasa wa Zaka za Kazi wenye wafuasi Zaidi ya watu 375,000.
Katika chapisho lake ndugu Zaka za Kazi ameweka vielelezo vinavyo thibitisha kauli yake hiyo kwakuwalaumu wadau wa soka nchini kwakuto fanya tafiti za kutosha.

“Hii ni changamoto kwa wadau wote wa soka nchini Tanzania; wachambuzi, waandishi wa habari, mamlaka za soka na serikali kwa maana ya wizara ya michezo na baraza la michezo.
Fanyeni utafiti na mje na majibu sahihi maana siku zinavyozidi kwenda, uongo unakuwa ukweli kwa sababu watu wanaamini yasiyo sahihi. “ Thabith Zakaria

Ameendelea kusimamia msimao wake kuhusu tafiti anazodai zinazopuuzwa na wadau wa soka nchi, Kwakupuuza taarifa muhimu.

“Ligi ya Tanzania ilianza mwaka 1965 ikiitwa Klabu Bingwa ya Taifa. Hadi mwaka huu, 2023, ni miaka 58.
Maana yake kuna mabingwa 58 wanatakiwa kuwepo. Sasa kama Yanga ni mabingwa mara 29, Simba mara 22 maana yake hawa wawili peke yao wamechukua ubingwa mara 51.
Katika misimu 58, imebaki misimu 7 pekee ambayo wamechukua wengine.
Hao wengine ni wafuatao:

Cosmopolitan -1 (1967)
Mseto -1 (1975)
Pan African – 1 (1982)
KMKM – 1 (1984)
Majimaji – 3 (1985, 1986 na 1998)
African Sports – 1 (1988)
Malindi – 2 (1989 na 1992)
Pamba – 1 (1990)
TZ Prisons – 1 (1999)
Azam FC – 1 (2014)”
Zaka Za kazi
Hata hivyo ndugu Thabith Zakaria ameahidi kuendelea kutoa taarifa Zaidi kuhusiana na hoja yake.
Nini maoni yako juu ya mjadala huu?
Mwandishi: John Mwonga.
Wamachinga.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram