243 views 2 mins 0 comments

WAZIRI SIMBACHAWENE AITAKA TAKUKURU ISIJIFUNGIE OFISINI, IENDE KWA JAMII

In KITAIFA
June 15, 2023


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka ofisini na kwenda sehemu ambako huduma za kijamii zinatolewa kwa kuwa huko kuna malalamiko mengi ya wananchi kuhusu kutoondewa haki katika kupata huduma.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma Waziri Simbachawene katika ziara yake ya kazi na Watumishi wa Taasisi hiyo kilicholenga kuhimiza uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao kwa maslahi mapana ya Taifa.

Aisha simbachawene Amesema ni wakati sasa wa TAKUKURU kwenda kupambana na rushwa katika maeneo hayo badala ya kukaa ofisini huku wakisubiri kupewa taarifa za rushwa na watu wengine.

“Naitaka TAKUKURU ya sasa iende huko kwa wananchi wasio na sauti wanakopatiwa huduma za kijamii zikiwemo ardhi, elimu, afya na nyinginezo lakini kuna kero kubwa ya rushwa,” waziri Simbachawene akisisitiza.

Ameongeza kuwa chombo hiki cha TUKUKURU kinatakiwa kiende sehemu zinakotolewa huduma za kijamii na kionekane kinafanya kazi ya kusikiliza, kunusa, kutazama, kugusa na kuwabaini wale wote wanaojenga mazingira ya rushwa kwa wananchi ili waweze kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria. 

“Yapo maeneo mengi ambayo tumeyaona ni ya kawaida lakini yanasababisha watoa huduma wetu kuingia katika rushwa, mangúniko ni mengi juu ya rushwa, hivyo ni lazima hatua zichukulie kudhibiti hili kwa maendeleo ya taifa,” waziri Simbachawene amesema.

Aidha, Mhe. Simbachawene amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha TAKUKURU kutekeleza majukumu yake kikamilifu, hivyo ni wakati sasa wa kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais kwa kufanya kazi kikamilifu katika kupamba na rushwa na kuitokomeza.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,  CP Salum Hamduni amesema TAKUKURU imeanza kufanya kazi zake kimkakati kutoka kufanya kazi kimazoea hadi kwenye kuhakikisha wananchi wanapewa huduma za kijamii pasipo kutengenezewa mazingira ya rushwa.

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram