118 views 2 mins 0 comments

Nchemba kunufaisha maendeleo ya jamii katika Bajeti

In KITAIFA
June 15, 2023

Waziri wa fedha na mpango Dkt Mwiguru Lameck Nchemba Leo amewasilisha Utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleo ya Mwaka 2022/23 Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23 ambao uliotengewa jumla ya shilingi bilioni 15,006.0, sawa na asilimia 36.2 ya Bajeti ya Serikali ambapo shilingi bilioni 12,306.9, sawa na asilimia 82.0 ya bajeti ya fedha za maendeleo ni fedha za ndani na shilingi bilioni 2,699.1, sawa na asilimia 18.0 ni fedha za nje.

Ridhaa ya matumizi ya fedha za maendeleo iliyotolewa katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Mei, 2023, ni shilingi bilioni 12,885.09 sawa na asilimia 93.67 ya lengo katika kipindi hicho. Kati ya kiasi hicho kilichotolewa, shilingi bilioni 11,145.51 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 1,739.58 ni fedha za nje.

Aidha Dkt Nchemba amesema baadhi ya maeneo ya kipaumbele yaliyopatiwa fedha za maendeleo katika kipindi husika ni kama yafuatayo.

Shilingi bilioni 1,164.34 kwa ajili ya Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Mto Rufiji – MW 2,115;

Shilingi bilioni 1,289.46 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge Railway);

Shilingi bilioni 1,151.11 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara kuu, barabara za mikoa, barabara za mijini na vijijini na madaraja;

Shilingi bilioni 652.1 kwa ajili ya kugharamia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu;

Shilingi bilioni 274.71 kwa ajili ya kuimarisha usafirishaji majini ikiwemo ujenzi na ukarabati wa bandari, ununuzi na ukarabati wa meli na vivuko katika bandari za maziwa makuu;

Shilingi bilioni 290.14 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji mijini na vijijini;

Shilingi bilioni 199.29 kwa ajili ya ukarabati wa Reli ya Kati (Mfuko wa Maendeleo ya Reli);

Shilingi bilioni 295.3 kwa ajili ya kugharamia elimu ya msingi na sekondari bila ada ikijumuisha mahitaji ya wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari za Serikali na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule, waratibu elimu kata na walimu wakuu;

Shilingi bilioni 202.51 kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA); na Shilingi bilioni 159.23 kwa ajili ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na chanjo za watoto kupitia MSD

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram