84 views 57 secs 0 comments

Nasredinne nabi kuachana na yanga rasmi

In MICHEZO
June 15, 2023

Uongozi wa yanga umetangaza rasmi kuachana na kocha wake nasredinne nabi baada ya kumaliza mkataba wake katika kikosi hicho.

Taarifa iliyotolewa na idara ya habari na mawasiliano wa kabla ya yanga imeeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo ulikutana na nabi na kuzungumza naye kuhusu kusaini mkataba mpya lakini nabi ameomba kupewa nafasi ya kwenda kutafuta changamoto mpya.

Akiwa kocha mkuu wa yanga nabi amefanikiwa kutwaa Mataji mawili ya ligi kuu ya NBC na Mataji mawili ya kombe la shirikisho la Azam na Mataji mawili ya ngao ya jamii na kuifikisha hatua ya fainali ya kombe la shirikisho la CAF.

Aidha uongozi wa yanga umeanza mchakato wa kumpata kocha mpya atayechukua nafasi ya kocha nasredinne nabi.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram