201 views 2 mins 0 comments

Mfumuko wa Bei ulivyoathiri Nchini

In KITAIFA
June 15, 2023

Mfumuko wa bei nchini umeendelea kuwa ndani ya lengo la wigo wa kuwa chini ya asilimia 5. Mwaka 2022, mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 4.3 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3

Aidha mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia mwezi Mei, 2023 umebaki kama ilivyokuwa kwa mwaka unaoishia mwezi Mei, 2022 ikiwa ni wastani wa asilimia 4.0. Hali hii imesababishwa na kuongezeka kwa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma;

Kwa kuongezeka kwa upatikanaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya maeneo nchini na nchi jirani kulikosababishwa na upatikanaji wa mvua katika maeneo yanayotegemea mvua.

Haya hivyo Katika kipindi kilichoishia mwezi Mei mwaka 2023, mfumuko wa bei wa vyakula na vinywaji baridi uliongezeka na kufikia asilimia 8.5 ikilinganishwa na asilimia 5.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2022.

Aidha mfumuko wa bei usiojumuisha vyakula na nishati (Core Inflation) ulifikia wastani wa asilimia 2.0 katika kipindi cha mwaka unaoishia mwezi Mei 2023 ikilinganishwa na asilimia 3.0 katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Kupungua kwa kasi ya upandaji bei ya bidhaa zisizo za vyakula na nishati kulitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa hizi nchini, ikiwemo saruji (Kielelezo Na. 1).

Kwa upande mwingine Nchemba amesema mfumuko wa bei wa nishati, mafuta na ankara za maji ulipungua kutoka asilimia 13.5 katika kipindi cha mwaka unaoishia mwezi Mei 2022 na kufikia asilimia hasi 1.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Mei 2023. Hii ilitokana na kupungua kidogo kwa bei ya nishati ya mafuta katika soko la dunia, mfano; kwa mwaka unaoishia mwezi Mei 2022, bei ya dizeli ilipanda kwa asilimia 18.7, petroli asilimia 10.8 na mafuta ya taa kwa asilimia 14.2.

Aidha Nchemba ameongeza kwa mwaka unaoishia mwezi Mei 2023, bei ya dizeli ilishuka hadi kufikia wastani wa asilimia hasi 0.3, petroli kwa asilimia chanya 1.9 na mafuta ya taa kwa asilimia hasi 2.1

/ Published posts: 1209

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram